Zaburi 64:1-10

  • Ulinzi dhidi ya mashambulizi yaliyofichika

    • “Mungu atawapiga mishale” (7)

Kwa kiongozi. Muziki wa Daudi. 64  Ee Mungu, sikia sauti yangu ninapokusihi.+ Ulinde uhai wangu kutokana na hofu ya adui.   Nikinge kutokana na njama za siri za waovu,+Kutoka kwa umati wa watenda maovu.   Wanaunoa ulimi wao kama upanga;Wanayalenga maneno yao ya ukatili kama mishale,   Ili wampige mtu asiye na hatia wakiwa mafichoni;Wanampiga ghafla, bila kuogopa.   Wanashikamana sana na kusudi lao ovu;*Wanazungumzia jinsi ya kuficha mitego yao. Wanasema: “Ni nani atakayeiona?”+   Wanatafuta njia mpya za kutenda uovu;Wanatunga kwa siri mbinu zao za ujanja;+Fikira zilizo ndani ya moyo wa kila mmoja wao hazieleweki kamwe.   Lakini Mungu atawapiga mishale;+Watajeruhiwa kwa ghafla na mshale.   Ulimi wao wenyewe utasababisha waanguke;+Wote wanaowatazama watatikisa kichwa.   Ndipo watu wote wataogopa,Nao watatangaza mambo ambayo Mungu ametenda,Nao watayafahamu matendo yake.+ 10  Mwadilifu atashangilia kwa sababu ya Yehova na kumkimbilia;+Wote walio wanyoofu moyoni watashangilia.*

Maelezo ya Chini

Au “Wanatiana moyo kutenda uovu.”
Au “watajigamba.”