Zaburi 129:1-8

  • Ashambuliwa lakini hakushindwa

Wimbo wa Safari za Kupanda. 129  “Wamenishambulia daima tangu nilipokuwa kijana”+ —Watu wa Israeli na waseme sasa—   “Wamenishambulia daima tangu nilipokuwa kijana;+Lakini hawajanishinda.+   Wale wanaolima kwa jembe la plau wamelima mgongoni mwangu;+Wameirefusha mitaro yao.”   Lakini Yehova ni mwadilifu;+Amezikatakata kamba za waovu.+   Wataaibishwa na kukimbia kwa fedheha,Wale wote wanaolichukia Sayuni.+   Watakuwa kama majani juu ya paaYanayonyauka kabla hayajang’olewa,   Ambayo hayawezi kujaa mkononi mwa mvunajiWala mikononi mwa yule anayekusanya masuke.   Wale wanaopita karibu nao hawatasema: “Baraka ya Yehova na iwe juu yenu;Tunawabariki katika jina la Yehova.”

Maelezo ya Chini