Zaburi 131:1-3

  • Kuridhika kama mtoto aliyeachishwa kunyonya

    • Kutotafuta mambo makubwa sana (1)

Wimbo wa Safari za Kupanda. Wa Daudi. 131  Ee Yehova, moyo wangu hauna kiburi,Wala macho yangu hayana majivuno;+Wala sijitafutii mambo makubwa sana,+Wala mambo yanayopita uwezo wangu.   Hasha, badala yake nimeituliza na kuinyamazisha nafsi yangu*+Kama mtoto aliyeachishwa kunyonya aliye na mama yake;Nimeridhika kama mtoto aliyeachishwa kunyonya.   Watu wa Israeli na wamngojee Yehova+Kuanzia sasa mpaka milele.

Maelezo ya Chini

Au “nimejituliza na kujinyamazisha mwenyewe.” Angalia Kamusi.