Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

A7-A

Matukio Muhimu Katika Maisha ya Yesu Duniani—Matukio Yaliyotangulia Huduma ya Yesu

Vitabu Vinne vya Injili Kulingana na Mfuatano wa Matukio

Chati zifuatazo zina ramani zinazoonyesha safari za kuhubiri za Yesu. Mishale kwenye ramani haionyeshi njia hususa aliyofuata badala yake inaonyesha alikoelekea.

Matukio Yaliyotangulia Huduma ya Yesu

WAKATI

MAHALI

TUKIO

MATHAYO

MARKO

LUKA

YOHANA

3 K.W.K.

Yerusalemu, hekalu

Malaika Gabrieli amtangazia Zekaria kuhusu kuzaliwa kwa Yohana Mbatizaji

   

1:5-25

 

Karibu 2 K.W.K.

Nazareti; Yudea

Malaika Gabrieli amtangazia Maria kuhusu kuzaliwa kwa Yesu; Maria amtembelea Elisabeti mtu wake wa ukoo

   

1:26-56

 

2 K.W.K.

Eneo lenye milima la Yudea

Yohana Mbatizaji azaliwa na kupewa jina; Zekaria atabiri; Yohana ataishi jangwani

   

1:57-80

 

2 K.W.K., karibu Okt. 1

Bethlehemu

Yesu azaliwa; “Neno akawa mwili”

1:1-25

 

2:1-7

1:1-5, 9-14

Karibu na Bethlehemu; Bethlehemu

Malaika awatangazia wachungaji habari njema; malaika wamsifu Mungu; wachungaji wamtembelea mtoto Yesu

   

2:8-20

 

Bethlehemu; Yerusalemu

Yesu atahiriwa (siku ya 8); wazazi wake wampeleka hekaluni (baada ya siku 40)

   

2:21-38

 

1 K.W.K. au 1 W.K.

Yerusalemu; Bethlehemu; Misri; Nazareti

Wanajimu wamtembelea; familia inakimbilia Misri; Herode awaua wavulana wadogo; familia yarudi kutoka Misri na waishi Nazareti

2:1-23

 

2:39, 40

 

12 W.K., Pasaka

Yerusalemu

Yesu mwenye umri wa miaka 12 akiwa hekaluni awauliza walimu maswali

   

2:41-50

 
 

Nazareti

Arudi Nazareti; aendelea kuwatii wazazi wake; ajifunza useremala; Maria apata watoto wa kiume wanne, na pia watoto wa kike (Mt 13:55, 56; Mk 6:3)

   

2:51, 52

 

29 W.K., majira ya kuchipua

Nyikani, Mto Yordani

Yohana Mbatizaji aanza huduma yake

3:1-12

1:1-8

3:1-18

1:6-8, 15-28