Idara ya Sheria
Anwani na namba za simu za idara yetu ya sheria.
Taarifa kwa Ajili ya Wanasheria
Habari kuhusu Mashahidi wa Yehova kwa ajili ya wataalamu wa mambo ya kisheria.
Articles
Mashahidi Zaidi Wafungwa Baada ya Uvamizi Mbaya wa Nyumba Nchini Urusi
Wenye mamlaka nchini Urusi wameendeleza kampeni yao ya kuwatisha, kuwakamata na kuwafunga Mashahidi kwa kushiriki utendaji wa imani yao.
Shahidi Mwingine wa Yehova Nchini Urusi Ashtakiwa kwa Madai ya Kuwa na Msimamo Mkali
Arkadya Akopyan, Shahidi mwenye umri wa miaka 70 ambaye amestaafu kazi ya kushona nguo, ni raia mnyoofu, anayetii sheria ambaye anataka kumwabudu Mungu kwa amani.
Mahakama ya Oryol Yasikiliza Ushahidi wa Kwanza wa Kesi ya Dennis Christensen
Bw. Christensen, amekuwa mahabusu tangu Mei 2017. Anaweza kukabili kifungo cha miaka sita hadi kumi gerezani kwa sababu tu ya kushiriki utendaji wake wa kidini.
Kampeni ya Kuwatisha Mashahidi wa Yehova Yaanza Nchini Urusi
Wenye mamlaka nchini Urusi wameyafungia mashirika ya kisheria ya Mashahidi wa Yehova, na sasa wameanza kuwashambulia Mashahidi na ibada yao.
Mashahidi Wawili Wazee Wamekufa Wakiwa Gerezani Nchini Eritrea
Habtemichael Tesfamariam na Habtemichael Mekonen walikufa wakiwa katika gereza la Mai Serwa mwanzoni mwa mwaka wa 2018. Wote walifungwa isivyo haki kwa sababu ya imani yao na walikabili hali mbaya katika gereza kwa karibu miaka kumi.
Teymur Akhmedov Ameachiliwa kwa Msamaha wa Rais
Rais wa Kazakhstan Nursultan Nazarbayev amempa msamaha Teymur Akhmedov, ambaye alikuwa amefungwa kwa zaidi ya mwaka mmoja kwa kuwaeleza wengine kuhusu imani yake ya dini. Msamaha huo umefuta rekodi yake ya uhalifu.
Turkmenistan Imepuuza Haki ya Uhuru wa Dhamiri
Mashahidi wawili wa Yehova wamehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja kwa kukataa kujiunga na utumishi wa kijeshi. Mpaka sasa Turkmenistan bado haitambui haki ya msingi ya wanaokataa kujiunga na utumishi wa kijeshi kwa sababu ya dhamiri na haina mpango wa utumishi wa badala wa kiraia.