Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

JW Library Lugha ya Ishara

JW Library Lugha ya Ishara

JW Library Lugha ya Ishara ni programu rasmi ya Mashahidi wa Yehova. Inaweza kupakua, kupanga, na kucheza video za lugha ya ishara zilizo kwenye Tovuti ya jw.org/sw.

 

Ni Nini Kipya

Julai 2022 (Toleo la 4.6)

  • Sehemu ya Yaliyomo imeboreshwa zaidi kwa ajili ya sehemu ya machapisho, kama vile kitabu Furahia Maisha Milele!

Januari 2022 (Toleo la 4.5)

  • Unaweza kushiriki viunganishi vya machapisho, maandiko, na video. Mpokeaji anaweza kufungua kiunganishi hicho moja kwa moja kwenye JW Library Sign Language.

  • Unaweza kushiriki video ambazo tayari zimepakuliwa.

  • Picha zilizoongezwa kwenye orodha zinaweza kuongezwa ukubwa.

  • Unaweza kuongeza picha na video nyingi kwenye orodha kwa wakati mmoja.

Agosti 2021 (Toleo la 4.4)

  • Picha ndogo zinajitokeza kwenye orodha ya alama ya kuchezesha video nazo zinaweza kupanuliwa zijaze skrini.

  • Vichwa, picha ndogo, na marejeo ya machapisho yanajitokeza kwenye orodha ya alama.

  • Makala za Mfululizo zinapatikana.

 

Ongeza Nafasi Kwenye Kifaa Chako

Jinsi ya kutumia vizuri nafasi uliyonayo.

Tumia Orodha

Unaweza kuongeza video, kupunguza urefu wa video au kupanga orodha jinsi ambavyo ungependa.

Njia Rahisi za Kucheza Video

Njia rahisi ya kucheza video kwa kutumia ishara kwenye skrini ya kugusa au kwa kubofya vitufe vya kibodi.

Sakinisha JW Library Sign Language Ikiwa Huwezi Kuipakua kwenye (App Store) Ukitumia Kifaa cha Android

Ikiwa huwezi kusakinisha JW Library Sign Language kwenye kifaa chako cha Android kutoka kwenye app store, unaweza kuisakinisha kwa kutumia Android Package Kit (APK).

Sakinisha JW Library Sign Language Ikiwa Huwezi Kuipakua Kwenye (App Store) Ukitumia Kifaa cha Windows

Ikiwa huwezi kusakinisha JW Library Sign Language kwenye kifaa chako cha Windows kutoka kwenye app store rasmi, unaweza kuisakinisha kwa kutumia faili za kusakinisha za JW Library Sign Language Windows.

Maswali Yanayoulizwa Mara Nyingi—JW Library Sign Language

Pata majibu ya maswali yanayoulizwa mara nyingi.