Mwanzo 5:1-32

5  Hiki ndicho kitabu cha historia ya Adamu. Siku ile Mungu alipomuumba Adamu alimfanya kwa mfano wa Mungu.+  Mwanamume na mwanamke aliwaumba.+ Baada ya hapo akawabariki, akawaita jina lao Mwanadamu+ siku ile walipoumbwa.+  Naye Adamu akaishi miaka 130. Ndipo akazaa mwana kwa mfano wake, kwa sura yake. Akamwita jina lake Sethi.+  Siku za Adamu baada ya kumzaa Sethi zikawa miaka 800. Wakati uleule akazaa wana na mabinti.+  Kwa hiyo siku zote ambazo Adamu aliishi zikajumlika kuwa miaka 930, naye akafa.+  Naye Sethi akaishi miaka 105. Ndipo akamzaa Enoshi.+  Na baada ya kumzaa Enoshi, Sethi akaishi miaka 807. Wakati uleule akazaa wana na mabinti.  Basi siku zote za Sethi zikawa miaka 912, naye akafa.  Enoshi akaishi miaka 90. Ndipo akamzaa Kenani.+ 10  Na baada ya kumzaa Kenani, Enoshi akaishi miaka 815. Wakati uleule akazaa wana na mabinti. 11  Basi siku zote za Enoshi zikawa miaka 905, naye akafa. 12  Naye Kenani akaishi miaka 70. Ndipo akamzaa Mahalaleli.+ 13  Na baada ya kumzaa Mahalaleli, Kenani akaishi miaka 840. Wakati uleule akazaa wana na mabinti. 14  Basi siku zote za Kenani zikawa miaka 910, naye akafa. 15  Naye Mahalaleli akaishi miaka 65. Ndipo akamzaa Yaredi.+ 16  Na baada ya kumzaa Yaredi, Mahalaleli akaishi miaka 830. Wakati uleule akazaa wana na mabinti. 17  Basi siku zote za Mahalaleli zikawa miaka 895, naye akafa. 18  Na Yaredi akaishi miaka 162. Ndipo akamzaa Enoko.+ 19  Na baada ya kumzaa Enoko, Yaredi akaishi miaka 800. Wakati uleule akazaa wana na mabinti. 20  Basi siku zote za Yaredi zikawa miaka 962, naye akafa. 21  Na Enoko akaishi miaka 65. Ndipo akamzaa Methusela.+ 22  Na baada ya kumzaa Methusela, Enoko akaendelea kutembea pamoja na Mungu wa kweli miaka 300. Wakati uleule akazaa wana na mabinti. 23  Basi siku zote za Enoko zikawa miaka 365. 24  Naye Enoko akaendelea kutembea+ pamoja na Mungu wa kweli.+ Kisha hakuwapo tena, kwa maana Mungu alimchukua.+ 25  Naye Methusela akaishi miaka 187. Ndipo akamzaa Lameki.+ 26  Na baada ya kumzaa Lameki, Methusela akaishi miaka 782. Wakati uleule akazaa wana na mabinti. 27  Basi siku zote za Methusela zikawa miaka 969, naye akafa. 28  Naye Lameki akaishi miaka 182. Ndipo akamzaa mwana. 29  Naye akamwita jina lake Noa,+ akisema: “Huyu atatuletea faraja katika kazi yetu na katika maumivu ya mikono yetu yanayoletwa na udongo ambao Yehova amelaani.”+ 30  Na baada ya kumzaa Noa, Lameki akaishi miaka 595. Wakati uleule akazaa wana na mabinti. 31  Basi siku zote za Lameki zikawa miaka 777, naye akafa. 32  Naye Noa akafikia umri wa miaka 500. Baada ya hapo Noa akazaa Shemu,+ Hamu+ na Yafethi.+

Maelezo ya Chini