Mwanzo 44:1-34

44  Baadaye akamwamuru mtu aliyekuwa akisimamia nyumba yake,+ akisema: “Ijaze mifuko ya watu hawa kwa chakula kwa kadiri wanavyoweza kuchukua. Utie pesa za kila mmoja wao katika kinywa cha mfuko wake.+  Lakini kiweke kikombe changu, kile kikombe cha fedha, katika kinywa cha mfuko wa yule mdogo zaidi pamoja na pesa za nafaka yake.” Basi akafanya kupatana na neno la Yosefu alilokuwa amesema.+  Asubuhi kulikuwa kumepambazuka watu hao waliporuhusiwa kuondoka,+ pamoja na punda zao.  Wakatoka nje ya jiji. Hawakuwa wameenda mbali wakati Yosefu alipomwambia mtu aliyekuwa akisimamia nyumba yake: “Ondoka! Wafuatilie watu hao nawe uhakikishe umewafikia na kuwaambia, ‘Kwa nini mmelipa ubaya kwa wema?+  Je, kikombe hiki sicho anachonywea bwana wangu na ambacho hutumia kusoma ishara za bahati kwa ustadi?+ Mmefanya kitendo kibaya.’”  Mwishowe akawafikia na kuwaambia maneno hayo.  Lakini wakamwambia: “Kwa nini bwana wangu anasema maneno kama hayo? Ni jambo lisilowaziwa kwamba watumishi wako wafanye lolote kama hilo.  Kwani, pesa tulizopata vinywani mwa mifuko yetu tulikurudishia kutoka nchi ya Kanaani.+ Basi, tungewezaje kuiba fedha au dhahabu katika nyumba ya bwana wako?+  Mtumwa wako atakayepatikana nacho na afe, nasi tuwe watumwa kwa bwana wangu.”+ 10  Ndipo akasema: “Basi sasa na iwe hivyo kama mlivyosema.+ Yule ambaye atapatikana kuwa nacho atakuwa mtumwa wangu,+ lakini ninyi mtakuwa hamna hatia.” 11  Kisha wakashusha chini upesi kila mmoja mfuko wake nao wakafungua kila mtu mfuko wake. 12  Naye akatafuta kwa uangalifu. Akaanzia kwa yule mkubwa zaidi na kumalizia kwa yule mdogo zaidi. Mwishowe kikombe kikapatikana katika mfuko wa Benyamini.+ 13  Kisha wakararua nguo zao za kujitanda,+ na kila mmoja akainua mzigo wake na kuurudisha juu ya punda wake, wakarudi jijini. 14  Naye Yuda+ na ndugu zake wakaenda mpaka nyumbani kwa Yosefu, naye bado alikuwamo; nao wakaanguka chini mbele yake.+ 15  Yosefu akawaambia: “Ni tendo gani hili mlilolifanya? Je, hamkujua kwamba mimi naweza kusoma ishara za bahati kwa ustadi?”+ 16  Yuda akajibu, akasema: “Tumwambie nini bwana wangu? Tuseme nini? Nasi tunaweza kuonyeshaje kuwa sisi ni waadilifu?+ Mungu wa kweli amegundua kosa la watumwa wako.+ Tazama sisi ni watumwa wa bwana wangu,+ sisi na yule ambaye mkononi mwake kikombe kilipatikana!” 17  Lakini yeye akasema: “Ni jambo lisilowaziwa upande wangu kufanya hivyo!+ Mtu ambaye mkononi mwake kikombe hicho kilipatikana ndiye atakayekuwa mtumwa wangu.+ Ninyi wengine, nendeni kwa amani kwa baba yenu.”+ 18  Sasa Yuda akamkaribia, akamwambia: “Nakuomba, bwana wangu, tafadhali mruhusu mtumwa wako aongee neno masikioni mwa bwana wangu,+ wala usiache hasira+ yako iwake juu ya mtumwa wako, kwa sababu wewe ni kama Farao.+ 19  Bwana wangu aliwauliza watumwa wake, akisema, ‘Je, mna baba au ndugu?’ 20  Basi tukamwambia bwana wangu, ‘Tuna baba aliye mzee na mtoto wa uzee wake, aliye mdogo zaidi.+ Lakini ndugu yake amekufa hivi kwamba yeye tu ndiye aliyesalia wa mama yake,+ na baba yake anampenda.’ 21  Kisha ukawaambia watumwa wako, ‘Mleteni kwangu nipate kumwona.’+ 22  Lakini tukamwambia bwana wangu, ‘Mvulana huyo hawezi kumwacha baba yake. Akimwacha, bila shaka baba yake atakufa.’+ 23  Halafu ukawaambia watumwa wako, ‘Ndugu yenu mdogo asiposhuka pamoja nanyi, msiuone uso wangu tena kamwe.’+ 24  “Basi tukaenda kwa mtumwa wako, baba yangu, tukamwambia maneno ya bwana wangu. 25  Baadaye baba yetu akasema, ‘Rudini, mkatununulie chakula kidogo.’+ 26  Lakini tukamwambia, ‘Hatuwezi kwenda. Ikiwa ndugu yetu mdogo yuko pamoja nasi tutaenda, kwa sababu hatuwezi kuuona uso wa mtu huyo ikiwa ndugu yetu mdogo hayuko pamoja nasi.’+ 27  Kisha mtumwa wako, baba yangu, akatuambia, ‘Ninyi wenyewe mnajua vizuri kwamba mke wangu alinizalia wana wawili tu.+ 28  Baadaye mmoja aliniacha nami nikasema: “Ah, haikosi ameraruliwa vipande-vipande!”+ nami sijamwona mpaka leo hii. 29  Mkimchukua huyu naye toka machoni pangu na apatwe na tukio lenye kufisha, bila shaka mtazishusha mvi zangu kwa msiba mpaka katika Kaburi.’*+ 30  “Sasa basi, nikifika tu kwa mtumwa wako, baba yangu, bila mvulana huyu, na hali nafsi yake imeshikamana na nafsi ya mvulana huyu,+ 31  basi bila shaka itatukia kwamba mara atakapoona kwamba huyu mvulana hayupo atakufa tu, na watumwa wako kwa kweli watazishusha mvi za mtumwa wako baba yetu kwa huzuni mpaka katika Kaburi.* 32  Kwa maana mtumwa wako alijitoa kuwa dhamana+ ya mvulana huyu awapo mbali na baba yake, akisema, ‘Nisipomrudisha kwako, basi nitakuwa nimemtendea baba yangu dhambi milele.’+ 33  Tafadhali sasa, basi, mtumwa wako na abaki akiwa mtumwa badala ya huyu mvulana ili apate kwenda na ndugu zake.+ 34  Kwa maana ninawezaje kwenda kwa baba yangu bila yeye nisije nikautazama msiba utakaompata baba yangu?”+

Maelezo ya Chini

Sheoli. Tazama Nyongeza 4.
Sheoli. Tazama Nyongeza 4.