Mwanzo 11:1-32

11  Sasa dunia yote iliendelea kuwa na lugha moja na maneno ya namna moja.  Mwishowe ikawa kwamba walipokuwa wakisafiri kuelekea mashariki, waligundua nchi tambarare ya bondeni katika nchi ya Shinari,+ nao wakakaa huko.  Nao wakaanza kuambiana: “Haya! Na tutengeneze matofali tuyachome.” Basi matofali yakawa mawe yao, lakini lami ikawa saruji yao.+  Ndipo wakasema: “Haya! Na tujijengee jiji na pia mnara na kilele chake kiwe mbinguni,+ na tujifanyie jina maarufu,+ tusije tukatawanyika juu ya uso wote wa dunia.”+  Yehova akashuka aone jiji na mnara ambao wanadamu walikuwa wamejenga.+  Halafu Yehova akasema: “Tazama! Wao ni kikundi kimoja cha watu na wote wana lugha moja,+ na hivi ndivyo wanavyoanza kufanya. Basi sasa hakuna chochote wanachowazia akilini mwao kufanya kitakachowashinda kufikia.+  Haya! Na tushuke,+ tuvuruge+ lugha yao huko ili wasiweze kusikilizana lugha.”+  Basi Yehova akawatawanya juu ya uso wote wa dunia kutoka huko,+ nao pole kwa pole wakaacha kulijenga lile jiji.+  Hiyo ndiyo sababu liliitwa jina lake Babeli,+ kwa sababu huko ndiko Yehova alikuwa amevuruga lugha ya dunia yote, na kutoka huko Yehova alikuwa amewatawanya+ juu ya uso wote wa dunia. 10  Hii ndiyo historia ya Shemu.+ Shemu alikuwa na umri wa miaka 100 wakati alipomzaa Arpakshadi+ miaka miwili baada ya gharika. 11  Na baada ya kumzaa Arpakshadi, Shemu akaishi miaka 500. Wakati uleule akazaa wana na mabinti.+ 12  Naye Arpakshadi akaishi miaka 35. Ndipo akamzaa Shela.+ 13  Na baada ya kumzaa Shela, Arpakshadi akaishi miaka 403. Wakati uleule akazaa wana na mabinti. 14  Naye Shela akaishi miaka 30. Ndipo akamzaa Eberi.+ 15  Na baada ya kumzaa Eberi, Shela akaishi miaka 403. Wakati uleule akazaa wana na mabinti. 16  Naye Eberi akaishi miaka 34. Ndipo akamzaa Pelegi.+ 17  Na baada ya kumzaa Pelegi, Eberi akaishi miaka 430. Wakati uleule akazaa wana na mabinti. 18  Naye Pelegi akaishi miaka 30. Ndipo akamzaa Reu.+ 19  Na baada ya kumzaa Reu, Pelegi akaishi miaka 209. Wakati uleule akazaa wana na mabinti. 20  Naye Reu akaishi miaka 32. Ndipo akamzaa Serugi.+ 21  Na baada ya kumzaa Serugi, Reu akaishi miaka 207. Wakati uleule akazaa wana na mabinti. 22  Naye Serugi akaishi miaka 30. Ndipo akamzaa Nahori.+ 23  Na baada ya kumzaa Nahori, Serugi akaishi miaka 200. Wakati uleule akazaa wana na mabinti. 24  Naye Nahori akaishi miaka 29. Ndipo akamzaa Tera.+ 25  Na baada ya kumzaa Tera, Nahori akaishi miaka 119. Wakati uleule akazaa wana na mabinti. 26  Naye Tera akaishi miaka 70, kisha akamzaa Abramu,+ Nahori+ na Harani. 27  Na hii ndiyo historia ya Tera. Tera akamzaa Abramu, Nahori na Harani; naye Harani akamzaa Loti.+ 28  Baadaye Harani akafa akiwa angali na baba yake Tera katika nchi ya kuzaliwa kwake, katika Uru+ la Wakaldayo.+ 29  Nao Abramu na Nahori wakajichukulia wake. Jina la mke wa Abramu lilikuwa Sarai,+ na jina la mke wa Nahori lilikuwa Milka+ binti ya Harani, baba ya Milka na baba ya Iska. 30  Lakini Sarai aliendelea kuwa tasa;+ hakuwa na mtoto. 31  Baada ya hapo Tera akamchukua mwana wake Abramu, na mjukuu wake Loti,+ mwana wa Harani, na binti-mkwe wake Sarai,+ mke wa mwana wake Abramu, nao wakaondoka Uru la Wakaldayo pamoja naye ili kwenda katika nchi ya Kanaani.+ Baadaye wakaja Harani+ na kukaa huko. 32  Na siku za Tera zikawa miaka 205. Ndipo Tera akafa huko Harani.

Maelezo ya Chini