Utangulizi wa Sehemu ya 7

Utangulizi wa Sehemu ya 7

Sehemu hii inazungumzia historia ya maisha ya Mfalme Sauli na Mfalme Daudi, kwa kipindi cha miaka 80 hivi. Mwanzoni, Sauli alikuwa mnyenyekevu na alimwogopa Mungu, lakini baada ya muda alibadilika na kukataa kufuata mwongozo wa Yehova. Yehova alimkataa, na baada ya muda akamwagiza Samweli amtie mafuta Daudi ili awe mfalme wa Israeli. Kwa sababu ya wivu, Sauli alijaribu mara nyingi kumuua Daudi, hata hivyo, Daudi hakulipiza kisasi. Yonathani, mwana wa Sauli, alijua kwamba Yehova alikuwa amemchagua Daudi, hivyo akawa mshikamanifu kwa Daudi. Ingawa Daudi alifanya dhambi nzito, alikubali nidhamu ya Yehova. Ikiwa wewe ni mzazi, msaidie mtoto wako kutambua umuhimu wa kuunga mkono mipango ya Mungu.

KATIKA SEHEMU HII

SOMO LA 39

Mfalme wa Kwanza wa Israeli

Ingawa Yehova alikuwa amewapa Waisraeli waamuzi wa kuwaongoza, bado walitaka wawe na mfalme. Samweli alimtia mafuta Sauli awe mfalme wa kwanza wa Israeli, lakini baadaye Yehova alimkataa Sauli. Kwa nini?

SOMO LA 40

Daudi na Goliathi

Yehova anamchagua Daudi kuwa mfalme wa Israeli anayefuata, na Daudi anaonyesha kwa nini huo ulikuwa uchaguzi unaofaa.

SOMO LA 41

Daudi na Sauli

Kwa nini mwanamume mmoja alimchukia mwenzake, na yule aliyechukiwa alitendaje?

SOMO LA 42

Yonathani Alikuwa Jasiri na Mshikamanifu

Mwana wa mfalme alikuwa rafiki wa karibu wa Daudi.

SOMO LA 43

Dhambi ya Mfalme Daudi

Uamuzi mbaya unaleta matatizo mengi sana.