Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Utangulizi wa Sehemu ya 2

Utangulizi wa Sehemu ya 2

Kwa nini Yehova alileta gharika na kuharibu ulimwengu wa wakati huo? Mwanzoni mwa historia ya wanadamu, kulitokea ushindani kati ya wema na uovu. Baadhi ya watu, kama vile Adamu, Hawa, na mtoto wao Kaini, walichagua kufanya mambo mabaya. Watu wachache kama vile Abeli na Noa, walichagua kufanya mema. Watu wengi walikuwa wabaya sana hivi kwamba Yehova aliamua kuleta mwisho wa ulimwengu huo mwovu. Sehemu hii itatusaidia kujifunza jinsi Yehova anavyohisi kuhusu maamuzi tunayofanya na kwamba hataruhusu kamwe uovu ushinde wema.

KATIKA SEHEMU HII

Adamu na Hawa Hawakumtii Mungu

Kwa nini mti mmoja ulikuwa wa pekee katika bustani ya Edeni? Kwa nini Hawa alikula tunda la mti huo?

Hasira Yasababisha Mauaji

Mungu alikubali dhabihu ya Abeli lakini aliikataa dhabihu ya Kaini. Kaini alipojua hilo alikasirika sana na akafanya jambo baya.

Safina ya Noa

Malaika walipokuja duniani na kujichukulia wanawake, walizaa watoto ambao walikuwa majitu. Jeuri ilienea kotekote. Lakini Noa alikuwa tofauti​—alimpenda na kumtii Mungu.

Watu Nane Waliokoka na Kuingia Katika Ulimwengu Mpya

Mvua ya Gharika ilinyesha kwa siku 40 mchana na usiku. Noa na familia yake walikaa ndani ya safina kwa zaidi ya mwaka mmoja. Hatimaye, Mungu aliwaambia watoke katika safina.