Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Utangulizi wa Sehemu ya 13

Utangulizi wa Sehemu ya 13

Yesu alikuja duniani ili kutoa uhai wake kwa ajili ya wanadamu wasio wakamilifu. Ingawa alikufa, yeye aliushinda ulimwengu. Yehova alikuwa mshikamanifu kwa Mwana wake, hivyo alimfufua. Alipokuwa hai hapa duniani, Yesu aliwatumikia watu kwa unyenyekevu na kuwasamehe walipokosea. Baada ya kufufuliwa, Yesu aliwatokea wanafunzi wake. Aliwafundisha jinsi ya kufanya kazi muhimu aliyokuwa amewapa. Ikiwa wewe ni mzazi, msaidie mtoto wako kuelewa kwamba sisi pia tunapaswa kushiriki katika kazi hiyo.

KATIKA SEHEMU HII

Mlo wa Mwisho wa Yesu

Yesu aliwapa mitume wake maagizo muhimu wakati wa mlo wao wa mwisho.

Yesu Akamatwa

Yuda Iskariote aliongoza umati wa watu wenye marungu na mapanga ili wamkate Yesu.

Petro Anamkana Yesu

Ni nini kilichotendeka katika ua wa nyumba ya Kayafa? Yesu alitendewa jinsi gani ndani ya nyumba?

Yesu Afa huko Golgotha

Kwa nini Pilato anaamuru Yesu auawe?

Yesu Afufuliwa

Ni mambo gani yenye kupendeza yanayotokea baada ya Yesu kuuawa?

Yesu Awatokea Wavuvi

Anafanya nini ili wamtambue?

Yesu Arudi Mbinguni

Lakini kabla ya kufanya hivyo, anawapa wanafunzi wake maagizo muhimu sana.