Isaya 34:1-17

  • Kisasi cha Yehova dhidi ya mataifa (1-8)

  • Edomu itafanywa ukiwa (9-17)

34  Njooni karibu ili msikie, enyi mataifa,Na msikilize, enyi watu. Dunia na vyote vinavyoijaza na visikilize,Nchi na mazao yake yote.   Kwa maana hasira ya Yehova inawaka dhidi ya mataifa yote,+Na ghadhabu yake dhidi ya jeshi lao lote.+ Atawaangamiza;Atawachinja.+   Watu wao waliouawa watatupwa nje,Na uvundo wa maiti zao utapaa;+Milima itayeyuka kwa sababu ya* damu yao.+   Jeshi lote la mbinguni litaoza kabisa,Na mbingu zitakunjwa kama kitabu cha kukunjwa. Jeshi lake lote litanyauka kabisa,Kama jani lililonyauka linavyoanguka kutoka kwenye mzabibuNa tini iliyonyauka kutoka kwenye mtini.   “Kwa maana upanga wangu utaloweshwa mbinguni.+ Utashuka juu ya Edomu katika hukumu,+Juu ya watu ambao niliamua kuwaangamiza.   Yehova ana upanga; utafunikwa kwa damu. Utafunikwa kwa mafuta,+Kwa damu ya wanakondoo dume na mbuzi,Kwa mafuta ya figo za kondoo dume. Kwa maana Yehova ana dhabihu kule Bosra,Machinjo makubwa katika nchi ya Edomu.+   Fahali mwitu watashuka pamoja nao,Ng’ombe dume wachanga watashuka pamoja na wenye nguvu. Nchi yao itajaa damu,Na mavumbi yao yatalowa mafuta.”   Kwa maana Yehova ana siku ya kisasi,+Mwaka wa malipo ya kesi dhidi ya Sayuni.+   Vijito vyake* vitabadilishwa kuwa lami,Na mavumbi yake kuwa kiberiti,Na nchi yake itakuwa kama lami inayowaka. 10  Haitazimwa usiku wala mchana;Moshi wake utaendelea kupaa milele. Itabaki ukiwa kizazi baada ya kizazi;Hakuna yeyote atakayepita katikati yake milele na milele.+ 11  Mwari na nungunungu wataimiliki,Na bundi wenye masikio marefu na kunguru watakaa ndani yake. Atanyoosha juu yake kamba ya kupimia ya utupuNa timazi* ya ukiwa. 12  Hakuna yeyote kati ya watu wake mashuhuri atakayepewa ufalme,Na wakuu wake wote watakuwa si kitu. 13  Miiba itaota katika minara yake yenye ngome,Upupu na magugu yenye miiba katika ngome yake. Nchi hiyo itakuwa makao ya mbwamwitu,+Boma la mbuni. 14  Viumbe wa jangwani watakutana na wanyama wanaopiga mayowe,Na mbuzi wa mwituni* atamwita mwenzake. Naam, huko babewatoto atakaa na kupata mahali pa kupumzika. 15  Nyoka-pili atatengeneza kiota chake huko na kutaga mayai,Naye atayaangua na kuyakusanya katika kivuli chake. Naam, vipanga watakusanyika huko, kila mmoja na mwenzake. 16  Tafuteni katika kitabu cha Yehova na mkisome kwa sauti: Hakuna hata mmoja wao atakayekosekana;Hakuna hata mmoja wao atakayekosa mwenzake,Kwa maana kinywa cha Yehova ndicho kimeamuru,Na roho yake ndiyo imewakusanya pamoja. 17  Yeye Ndiye amewapigia kura,Na mkono wake mwenyewe umewapimia mahali walipogawiwa.* Wataimiliki daima;Watakaa ndani yake kwa vizazi vyote.

Maelezo ya Chini

Au “itatiririka.”
Inaonekana vinarejelea Bosra, jiji kuu la Edomu.
Tnn., “mawe.”
Au labda, “Na roho waovu walio kama mbuzi.”
Tnn., “umewagawia kwa kamba ya kupimia.”