Isaya 16:1-14

  • Ujumbe dhidi ya Moabu waendelea (1-14)

16  Pelekeni kondoo dume kwa mtawala wa nchi,Kutoka Sela kupitia nyikaniMpaka kwenye mlima wa binti ya Sayuni.   Kama ndege aliyefukuzwa kwenye kiota chake,+Ndivyo mabinti wa Moabu watakavyokuwa kwenye vivuko vya Arnoni.+   “Toeni shauri, tekelezeni uamuzi. Fanya kivuli chako cha adhuhuri kiwe kama usiku. Wafiche waliotawanyika na usiwasaliti wale wanaokimbia.   Watu wangu waliotawanyika na wakae ndani yako, Ee Moabu. Uwe maficho kwao kwa sababu ya mwangamizaji.+ Mkandamizaji ataufikia mwisho wake,Uharibifu utafikia mwisho,Na wale wanaowakanyaga wengine wataangamia kutoka duniani.   Kisha kiti cha ufalme kitaimarishwa kabisa katika upendo mshikamanifu. Yule anayekikalia katika hema la Daudi atakuwa mwaminifu;+Atahukumu kwa haki na kutekeleza uadilifu upesi.”+   Tumesikia kuhusu kiburi cha Moabu—ana kiburi sana+Majivuno yake na kiburi chake na ghadhabu yake;+Lakini maneno yake matupu yatakuwa ya bure.   Basi Moabu atamwombolezea Moabu;Wote wataomboleza.+ Wale waliopigwa wataomboleza kwa sababu ya keki za zabibu kavu za Kir-haresethi.+   Kwa maana matuta ya Heshboni+ yamenyauka. Mzabibu wa Sibma,+Watawala wa mataifa wameyakanyaga matawi yake mekundu sana;*Walikuwa wamefika mpaka Yazeri;+Walikuwa wameenea mpaka nyikani. Machipukizi yake yalikuwa yameenea mpaka baharini.   Hiyo ndiyo sababu nitaulilia mzabibu wa Sibma kama ninavyolilia Yazeri. Machozi yangu yatakulowesha ewe Heshboni na Eleale,+Kwa sababu vigelegele vya matunda yako ya kiangazi na vya mavuno yako vimekoma.* 10  Furaha na shangwe zimeondolewa katika shamba la matunda,Na hakuna nyimbo za shangwe au vigelegele katika mashamba ya mizabibu.+ Anayekanyaga hakanyagi tena divai katika mashinikizo,Kwa maana nimekomesha vigelegele.+ 11  Ndiyo sababu nina msukosuko ndani yangu kwa ajili ya Moabu,+Kama kinubi kinapopigwa,Na sehemu yangu ya ndani kabisa kwa ajili ya Kir-haresethi.+ 12  Hata Moabu akijichosha mahali pa juu na kwenda kusali katika patakatifu pake, hatatimiza lolote.+ 13  Hilo ndilo neno ambalo Yehova alisema awali kuhusu Moabu. 14  Na sasa Yehova anasema: “Katika muda wa miaka mitatu, kama miaka ya kibarua,* utukufu wa Moabu utafedheheshwa kwa vurugu nyingi za kila aina, na wale watakaobaki watakuwa wachache sana na wanyonge.”+

Maelezo ya Chini

Au “matawi yake yaliyojaa zabibu nyekundu.”
Au labda, “Kwa sababu kelele za vita zimeshuka juu ya matunda yako ya kiangazi na mavuno yako.”
Au “iliyohesabiwa kwa uangalifu kama kibarua anavyofanya”; yaani, kwa miaka mitatu kamili.