Ayubu 40:1-24

  • Yehova amuuliza maswali zaidi (1-24)

    • Ayubu akiri hana la kusema (3-5)

    • “Je, utatilia shaka haki yangu?” (8)

    • Mungu aeleza kuhusu nguvu za Behemothi (15-24)

40  Yehova akaendelea kumjibu Ayubu:   “Je, mtu anayetafuta makosa anapaswa kushindana na Mweza-Yote?+ Acha yule anayetaka kumkaripia Mungu ajibu.”+  Ayubu akamjibu Yehova:   “Tazama! Mimi sistahili.+ Nitakujibu nini? Ninafunika kinywa changu kwa mkono.+   Niliongea mara moja, lakini sitajibu tena;Mara mbili, lakini sitaongea tena.”   Kisha Yehova akamjibu Ayubu kutoka katika dhoruba ya upepo:+   “Tafadhali, jitayarishe* kama mwanamume;Nitakuuliza maswali, nawe unijibu.+   Je, utatilia shaka* haki yangu? Je, utanishutumu ili uwe mwadilifu?+   Je, una mkono wenye nguvu kama mkono wa Mungu wa kweli,+Au je, sauti yako inaweza kunguruma kama yake?+ 10  Tafadhali, jipambe kwa utukufu na ukuu;Jivike heshima na fahari. 11  Mwaga ghadhabu ya hasira yako;Mtazame kila mwenye kiburi, umshushe chini. 12  Mtazame kila mwenye kiburi, umnyenyekeze,Na uwakanyage waovu mahali wanaposimama. 13  Wafiche wote mavumbini;Wafunge* mahali palipofichika, 14  Ndipo hata mimi nitakapokiri mbele yako*Kwamba mkono wako wa kulia unaweza kukuokoa. 15  Tazama, huyu ni Behemothi* niliyemuumba kama nilivyokuumba. Yeye hula majani kama ng’ombe dume. 16  Tazama nguvu zilizo kiunoni mwakeNa nguvu zilizo katika misuli ya tumbo lake! 17  Huukaza mkia wake kama mwerezi;Kano za mapaja yake zimefumwa pamoja. 18  Mifupa yake ni mabomba ya shaba;Miguu yake ni kama fito za chuma kilichofuliwa. 19  Yeye ni wa kwanza miongoni mwa kazi za Mungu;Ni Muumba wake tu anayeweza kumkaribia kwa upanga wake. 20  Kwa maana milima huzalisha chakula kwa ajili yake,Ambako wanyama wote wa mwituni hucheza. 21  Hulala chini ya miti ya miyungiyungi,Kwenye kivuli cha matete mahali penye umajimaji. 22  Miti ya miyungiyungi humfunika kwa kivuli,Na mierebi ya bondeni* humzunguka. 23  Mto unaposukasuka, yeye hashtuki. Haogopi hata maji ya Yordani+ yakifurika kinywani mwake. 24  Je, kuna yeyote anayeweza kumkamata akiwa macho,Au kumtoboa pua kwa kulabu?*

Maelezo ya Chini

Tnn., “jifunge.”
Au “utabatilisha.”
Tnn., “Zifunge nyuso zao.”
Au “nitakapokupongeza.”
Labda ni kiboko.
Au “korongoni.”
Tnn., “mtego.”