Ayubu 15:1-35

  • Elifazi azungumza kwa mara ya pili (1-35)

    • Adai kwamba Ayubu hamwogopi Mungu (4)

    • Asema Ayubu ana kimbelembele (7-9)

    • ‘Mungu hana imani na watakatifu wake’ (15)

    • ‘Anayeteseka ni mwovu’ (20-24)

15  Elifazi+ Mtemani akajibu:   “Je, mtu mwenye hekima atajibu kwa hoja zisizo na maana,*Au, je, atajaza tumbo lake upepo wa mashariki?   Kukaripia kwa maneno matupu ni jambo lisilo na maana,Na kuzungumza tu hakuna faida yoyote.   Kwa maana unafanya watu wasimwogope Mungu,Na kuwazuia wasitafakari kamwe kumhusu Mungu.   Kwa maana kosa lako linakufanya useme unayosema,*Nawe unachagua maneno ya hila.   Kinywa chako mwenyewe kinakuhukumu, wala si mimi;Midomo yako mwenyewe inatoa ushahidi dhidi yako.+   Je, wewe ndiye mwanadamu wa kwanza kuzaliwa,Au ulizaliwa kabla ya vilima?   Je, wewe husikiliza mazungumzo ya siri ya Mungu,Au ni wewe peke yako mwenye hekima?   Unajua nini ambacho sisi hatujui?+ Unaelewa nini ambacho sisi hatuelewi? 10  Watu wenye mvi na wazee wako miongoni mwetu,+Watu wenye umri mkubwa kuliko baba yako. 11  Je, hutosheki na faraja za Mungu,Au maneno ya upole unayoambiwa? 12  Kwa nini moyo wako unakupeperusha,Na kwa nini macho yako yanawaka kwa hasira? 13  Kwa maana unaifanya roho yako imkasirikie Mungu,Nawe unaruhusu maneno ya aina hiyo yatoke katika kinywa chako mwenyewe. 14  Mwanadamu anayeweza kufa ni nini hata awe safi,Au yeyote anayezaliwa na mwanamke ni nini hata awe mwadilifu?+ 15  Tazama! Hana imani na watakatifu wake,Na hata mbingu si safi machoni pake.+ 16  Sembuse mtu anayechukiza na aliyepotoka,+Mwanadamu anayekunywa uovu kama maji! 17  Nitakujulisha; nisikilize! Nitasimulia mambo niliyoona, 18  Mambo ambayo watu wenye hekima wamejifunza kutoka kwa baba zao,+Mambo ambayo hawakuficha. 19  Ni wao peke yao waliopewa nchi,Na hakuna mgeni aliyepita miongoni mwao. 20  Mtu mwovu huteseka siku zake zote,Miaka yote aliyotengewa mkandamizaji. 21  Masikio yake husikia sauti zenye kutisha;+Wakati wa amani, wavamizi humshambulia. 22  Haamini kwamba ataponyoka kutoka gizani;+Amekusudiwa kuuawa kwa upanga. 23  Hutangatanga akitafuta chakula*—kiko wapi? Anajua vizuri kwamba siku ya giza iko karibu. 24  Taabu na maumivu makali huendelea kumtisha;Humshinda nguvu kama mfalme aliye tayari kushambulia. 25  Kwa maana yeye huunyoosha mkono wake dhidi ya Mungu mwenyeweNa kujaribu kumpinga* Mweza-Yote; 26  Hukimbia kwa ukaidi kumshambulia Yeye,Akiwa na ngao yake nene, iliyo imara;* 27  Uso wake umefunikwa kwa mafuta,Na kiuno chake kimepanuka kwa mafuta; 28  Hukaa katika majiji yatakayoangamizwa,Katika nyumba ambazo hazitakaliwa na yeyote,Ambazo zitakuwa marundo ya mawe. 29  Hatatajirika, na mali zake hazitaongezeka,Wala vitu anavyomiliki havitaenea nchini. 30  Hatakimbia kutoka gizani;Mwali wa moto utakausha tawi lake,*Naye atatoweka kwa kishindo cha pumzi ya kinywa cha Mungu.*+ 31  Hapaswi kukengeushwa na kutumaini mambo yasiyo na thamani,Kwa sababu atakachopata badala yake hakitakuwa na thamani; 32  Hilo litatendeka kabla ya siku yake,Na matawi yake hayatasitawi kamwe.+ 33  Atakuwa kama mzabibu unaoangusha zabibu zake mbichi,Na kama mzeituni unaoangusha maua yake. 34  Kwa maana kusanyiko la watu wanaomkataa Mungu* ni tasa,+Na moto utateketeza mahema ya rushwa. 35  Wanatunga mimba ya matatizo na kuzaa uovu,Na tumbo lao la uzazi huzaa udanganyifu.”

Maelezo ya Chini

Au “kwa ujuzi wa ubatili.”
Au “kosa lako linakizoeza kinywa chako.”
Tnn., “mkate.”
Au “kujaribu kumshinda.”
Tnn., “ngao yenye mafundo manene.”
Yaani, tumaini lolote la kupona.
Tnn., “chake.”
Au “waasi imani.”