Ayubu 28:1-28
28 “Kuna mahali pa kuchimba fedhaNa mahali pa dhahabu wanayosafisha;+
2 Chuma hutolewa ardhini,Na shaba huyeyushwa* kutoka katika miamba.+
3 Mwanadamu hulishinda giza;Huchunguza kwa kina katika utusitusi na giza,Akitafuta mawe yenye madini.
4 Huzamisha bomba mbali na makao ya watu,Mahali paliposahauliwa, mbali na mahali ambapo watu wanatembea;Wanaume fulani hushuka wakining’inia kwa kamba.
5 Chakula hukua juu ardhini;Lakini chini, kuna msukosuko kama wa moto.*
6 Katika mawe hayo kuna yakuti,Na vumbi lake lina dhahabu.
7 Hakuna ndege awindaye anayejua njia ya kufika huko;Jicho la mwewe mweusi halijaiona.
8 Hakuna mnyama yeyote wa mwituni mwenye fahari aliyeikanyaga;Mwanasimba hajazunguka huko.
9 Mwanadamu hugonga mwamba mgumu kwa mkono wake;Huipindua milima kwenye misingi yake.
10 Huchimba mitaro ya maji+ kwenye mwamba;Macho yake huona kila kitu chenye thamani.
11 Huziba chemchemi za mitoNa kufichua vitu vilivyofichwa.
12 Lakini hekima—inaweza kupatikana wapi,+Na kiko wapi chanzo cha uelewaji?+
13 Hakuna mwanadamu anayetambua thamani yake,+Nayo haiwezi kupatikana katika nchi ya walio hai.
14 Vilindi vya maji vinasema, ‘Haimo ndani yangu!’
Nayo bahari inasema, ‘Haiko pamoja nami!’+
15 Haiwezi kununuliwa kwa dhahabu safi;Wala thamani yake haiwezi kupimwa kwa fedha.+
16 Haiwezi kununuliwa kwa dhahabu ya Ofiri+Wala kwa madini ya shohamu na yakuti yasiyopatikana kwa urahisi.
17 Dhahabu na kioo haviwezi kulinganishwa nayo;Wala haiwezi kubadilishwa kwa chombo cha dhahabu bora.*+
18 Marijani na fuwele hazistahili kutajwa,+Kwa maana mfuko uliojaa hekima una thamani kuliko mfuko uliojaa lulu.
19 Topazi+ ya Kushi haiwezi kulinganishwa nayo;Haiwezi kununuliwa hata kwa dhahabu safi.
20 Lakini hekima hutoka wapi,Na kiko wapi chanzo cha uelewaji?+
21 Imefichwa kutoka machoni pa kila kiumbe aliye hai+Na kufichwa kutoka kwa ndege wa angani.
22 Maangamizi na kifo husema,‘Masikio yetu yamesikia tu habari zake.’
23 Mungu anaelewa njia ya kuipata;Yeye peke yake ndiye anayejua inakokaa,+
24 Kwa maana yeye hutazama mpaka kwenye miisho ya dunia,Naye huona kila kitu chini ya mbingu.+
25 Alipoupa upepo nguvu*+Na kuyapima maji,+
26 Alipoiwekea mvua sheria+Na njia kwa ajili ya mawingu ya dhoruba yenye ngurumo,+
27 Kisha akaiona hekima na kuifafanua;Aliiimarisha na kuijaribu.
28 Naye akamwambia mwanadamu:
‘Tazama! Kumwogopa Yehova—hiyo ndiyo hekima,+Na kuepuka uovu ni uelewaji.’”+
Maelezo ya Chini
^ Tnn., “humwagwa.”
^ Inaonekana kwamba maneno haya yanahusu uchimbaji wa madini.
^ Au “iliyosafishwa.”
^ Tnn., “uzito.”