Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Kitabu cha Methali

Sura

Muhtasari wa Yaliyomo

 • 1

  • Kusudi la methali (1-7)

  • Hatari za marafiki wabaya (8-19)

  • Hekima ya kweli hupaza sauti hadharani (20-33)

 • 2

  • Thamani ya hekima (1-22)

   • Tafuta hekima kama hazina zilizofichika (4)

   • Uwezo wa kufikiri ni ulinzi (11)

   • Uasherati huleta msiba (16-19)

 • 3

  • Uwe na hekima na umtumaini Yehova (1-12)

   • Mheshimu Yehova kwa vitu vyenye thamani (9)

  • Hekima huleta furaha (13-18)

  • Hekima huleta usalama (19-26)

  • Mambo mema ya kuwatendea wengine (27-35)

   • Watendee wengine mema inapowezekana (27)

 • 4

  • Mafundisho ya baba yenye hekima (1-27)

   • Zaidi ya yote, pata hekima (7)

   • Epuka vijia vya uovu (14, 15)

   • Kijia cha waadilifu huzidi kung’aa (18)

   • “Ulinde moyo wako” (23)

 • 5

  • Onyo dhidi ya wanawake waasherati (1-14)

  • Shangilia pamoja na mke wako (15-23)

 • 6

  • Jihadhari kuhusiana na kutoa dhamana ya mkopo (1-5)

  • “Mwendee chungu, ewe mvivu” (6-11)

  • Mtu mwovu asiyefaa kitu (12-15)

  • Vitu saba ambavyo Yehova anachukia (16-19)

  • Jilinde dhidi ya mwanamke mwovu (20-35)

 • 7

  • Zishike amri za Mungu uishi (1-5)

  • Kijana mjinga atongozwa (6-27)

   • “Kama ng’ombe dume anayeenda machinjioni” (22)

 • 8

  • Hekima yaongea kama mtu (1-36)

   • ‘Mimi ni mwanzo kabisa wa kazi za Mungu’ (22)

   • ‘Nilikuwa kando ya Mungu nikiwa mfanyakazi stadi’ (30)

   • “Niliwapenda sana wanadamu” (31)

 • 9

  • Hekima ya kweli inatoa mwaliko (1-12)

   • “Nitafanya siku zako ziwe nyingi” (11)

  • Mwanamke mpumbavu awaalika watu (13-18)

   • “Maji yaliyoibwa ni matamu” (17)

 • METHALI ZA SULEMANI (10:1–24:34)

  • 10

   • Mwana mwenye hekima humfanya baba yake ashangilie (1)

   • Mikono yenye bidii huleta utajiri (4)

   • Kusema maneno mengi husababisha makosa (19)

   • Baraka ya Yehova hutajirisha (22)

   • Kumwogopa Yehova hurefusha maisha (27)

  • 11

   • Wenye kiasi wana hekima (2)

   • Mwasi imani huwaangamiza wengine (9)

   • “Washauri wengi huleta mafanikio” (14)

   • Mtu mkarimu atapata ufanisi (25)

   • Anayeutumaini utajiri wake ataanguka (28)

  • 12

   • Anayechukia karipio hana akili (1)

   • “Maneno yanayosemwa bila kufikiri huchoma kama upanga” (18)

   • Kusitawisha amani huleta shangwe (20)

   • Midomo inayosema uwongo humchukiza Yehova (22)

   • Mahangaiko huulemea moyo (25)

  • 13

   • Wanaotafuta ushauri wana hekima (10)

   • Tumaini likikawia huufanya moyo uwe mgonjwa (12)

   • Mjumbe mwaminifu huleta maponyo (17)

   • Kutembea na wenye hekima humfanya mtu awe na hekima (20)

   • Nidhamu huonyesha upendo (24)

  • 14

   • Moyo hujua uchungu wake wenyewe (10)

   • Njia inayoonekana kuwa sawa inaweza kusababisha kifo (12)

   • Mjinga huamini kila neno (15)

   • Tajiri ana marafiki wengi (20)

   • Moyo mtulivu huupa mwili uzima (30)

  • 15

   • Jibu la upole hutuliza hasira (1)

   • Macho ya Yehova yako kila mahali (3)

   • Sala ya mtu mnyoofu humfurahisha Mungu (8)

   • Mipango huvunjika watu wasiposhauriana (22)

   • Tafakari kabla ya kujibu (28)

  • 16

   • Yehova huchunguza nia (2)

   • Mkabidhi Yehova kazi zako (3)

   • Mizani ya unyoofu hutoka kwa Yehova (11)

   • Kiburi hutangulia kuanguka kwa kishindo (18)

   • Mvi ni taji la umaridadi (31)

  • 17

   • Usilipe uovu kwa wema (13)

   • Ondoka kabla ugomvi haujaanza (14)

   • Rafiki wa kweli hupenda nyakati zote (17)

   • “Moyo wenye shangwe ni dawa nzuri” (22)

   • Mtu mwenye utambuzi huyazuia maneno yake (27)

  • 18

   • Kujitenga na wengine ni jambo la kichoyo lisilo la hekima (1)

   • Jina la Yehova ni mnara wenye nguvu (10)

   • Mali ni ulinzi wa kuwaziwa tu (11)

   • Hekima ya kusikiliza pande zote mbili (17)

   • Rafiki hushikamana na mtu kwa ukaribu kuliko ndugu (24)

  • 19

   • Ufahamu hutuliza hasira (11)

   • Mke mgomvi ni kama paa linalovuja (13)

   • Mke mwenye busara hutoka kwa Yehova (14)

   • Mtie mtoto nidhamu wakati bado kuna tumaini (18)

   • Hekima ya kusikiliza mashauri (20)

  • 20

   • Divai ni mdhihaki (1)

   • Mvivu halimi katika majira ya baridi kali (4)

   • Mawazo ya mtu ni kama maji yenye kina (5)

   • Onyo dhidi ya kuapa haraka-haraka (25)

   • Utukufu wa vijana ni nguvu zao (29)

  • 21

   • Yehova huuelekeza moyo wa mfalme (1)

   • Haki ni bora kuliko dhabihu (3)

   • Bidii huleta mafanikio (5)

   • Asiyemsikiliza mtu wa hali ya chini hatasikilizwa (13)

   • Hakuna hekima katika kumpinga Yehova (30)

  • 22

   • Jina jema ni bora kuliko mali nyingi (1)

   • Mazoezi ya mapema ya mtoto yatadumu maisha yake yote (6)

   • Mvivu huogopa kwamba simba yuko nje (13)

   • Nidhamu huondoa ujinga (15)

   • Mfanyakazi stadi huwatumikia wafalme (29)

  • 23

   • Uwe na busara unapokubali mwaliko (2)

   • Usifuatie utajiri (4)

   • Utajiri unaweza kuruka mbali nawe (5)

   • Usiwe miongoni mwa walevi (20)

   • Kileo huuma kama nyoka (32)

  • 24

   • Usiwaonee wivu waovu (1)

   • Nyumba hujengwa kwa hekima (3)

   • Mwadilifu anaweza kuanguka lakini atainuka (16)

   • Usilipize kisasi (29)

   • Kusinzia huleta umaskini (33, 34)

 • METHALI ZA SULEMANI ZILIZONAKILIWA NA WATU WA MFALME HEZEKIA (25:1–29:27)

  • 25

   • Kutunza siri (9)

   • Maneno yaliyochaguliwa vizuri (11)

   • Kuheshimu faragha ya wengine (17)

   • Kukusanya makaa ya mawe juu ya kichwa cha adui (21, 22)

   • Habari njema ni kama maji baridi (25)

  • 26

   • Ufafanuzi kuwahusu watu wavivu (13-16)

   • Epuka ugomvi usiokuhusu (17)

   • Epuka mizaha inayodhuru (18, 19)

   • Pasipo na kuni, moto huzimika (20, 21)

   • Maneno ya mchongezi ni kama matonge matamu (22)

  • 27

   • Karipio kutoka kwa rafiki hunufaisha (5, 6)

   • Mwanangu, ufanye moyo wangu ushangilie (11)

   • Chuma hunoa chuma (17)

   • Lijue kundi lako (23)

   • Mali haidumu milele (24)

  • 28

   • Sala ya mtu asiyesikiliza inachukiza (9)

   • Anayeungama huonyeshwa rehema (13)

   • Anayeharakisha kupata utajiri hatakosa hatia (20)

   • Karipio ni bora kuliko kusifusifu (23)

   • Mtu mkarimu hakosi chochote (27)

  • 29

   • Mtoto aliyeachiliwa huleta aibu (15)

   • Bila maono, watu hutenda wapendavyo (18)

   • Mtu mwenye hasira huchochea ugomvi (22)

   • Mtu mnyenyekevu hupata utukufu (23)

   • Kuwaogopa wanadamu ni mtego (25)

 • 30

  • MANENO YA AGURI (1-33)

   • Usinipe umaskini wala utajiri (8)

   • Vitu visivyotosheka kamwe (15, 16)

   • Vitu visivyoacha alama (18, 19)

   • Mwanamke mzinzi (20)

   • Wanyama wenye hekima ya kisilika (24)

 • 31

  • MANENO YA MFALME LEMUELI (1-31)

   • Ni nani anayeweza kumpata mke mwema? (10)

   • Hufanya kazi kwa bidii na jitihada (17)

   • Fadhili ziko kwenye ulimi wake (26)

   • Watoto wake na mume wake humsifu (28)

   • Sura nzuri na urembo hutoweka upesi (30)