Hesabu 33:1-56

  • Vituo vya safari ya Waisraeli nyikani (1-49)

  • Maagizo ya kuteka nchi ya Kanaani (50-56)

33  Waisraeli walipiga kambi katika vituo vifuatavyo walipotoka nchini Misri+ kulingana na vikosi vyao*+ wakiongozwa na Musa na Haruni.+  Musa aliandika kila kituo katika safari yao kama Yehova alivyomwagiza, na hivi ndivyo vituo vya safari yao, kituo baada ya kituo:+  Waliondoka Ramesesi+ siku ya 15 ya mwezi wa kwanza.+ Siku hiyohiyo baada ya Pasaka,+ Waisraeli waliondoka kwa ujasiri* huku Wamisri wote wakiwatazama.  Wakati huo, Wamisri walikuwa wakiwazika wazaliwa wao wote wa kwanza ambao Yehova aliwaangamiza,+ kwa kuwa Yehova alikuwa ametekeleza hukumu dhidi ya miungu yao.+  Kwa hiyo Waisraeli wakaondoka Ramesesi na kupiga kambi Sukothi.+  Kisha wakaondoka Sukothi na kupiga kambi Ethamu,+ kwenye ukingo wa nyika.  Halafu wakaondoka Ethamu, wakageuka na kurudi Pihahirothi, mbele ya Baal-sefoni,+ wakapiga kambi karibu na Migdoli.+  Kisha wakaondoka Pihahirothi na kupita katikati ya bahari+ mpaka nyikani,+ wakaendelea kusafiri kwa siku tatu katika nyika ya Ethamu+ na kupiga kambi huko Mara.+  Kisha wakaondoka Mara na kufika Elimu. Huko Elimu kulikuwa na chemchemi 12 za maji na mitende 70, kwa hiyo wakapiga kambi mahali hapo.+ 10  Halafu wakaondoka Elimu na kupiga kambi kando ya Bahari Nyekundu. 11  Kisha wakaondoka kando ya Bahari Nyekundu na kupiga kambi katika nyika ya Sini.+ 12  Halafu wakaondoka katika nyika ya Sini na kupiga kambi Dofka. 13  Baadaye wakaondoka Dofka na kupiga kambi Alushi. 14  Kisha wakaondoka Alushi na kupiga kambi Refidimu,+ ambapo hapakuwa na maji ya kunywa. 15  Halafu wakaondoka Refidimu na kupiga kambi katika nyika ya Sinai.+ 16  Wakaondoka katika nyika ya Sinai na kupiga kambi Kibroth-hataava.+ 17  Kisha wakaondoka Kibroth-hataava na kupiga kambi Haserothi.+ 18  Baada ya hapo wakaondoka Haserothi na kupiga kambi Rithma. 19  Kisha wakaondoka Rithma na kupiga kambi Rimon-peresi. 20  Halafu wakaondoka Rimon-peresi na kupiga kambi Libna. 21  Wakaondoka Libna na kupiga kambi Risa. 22  Kisha wakaondoka Risa na kupiga kambi Kehelatha. 23  Halafu wakaondoka Kehelatha na kupiga kambi kwenye Mlima Sheferi. 24  Kisha wakaondoka kwenye Mlima Sheferi na kupiga kambi Harada. 25  Halafu wakaondoka Harada na kupiga kambi Makelothi. 26  Kisha wakaondoka+ Makelothi na kupiga kambi Tahathi. 27  Halafu wakaondoka Tahathi na kupiga kambi Tera. 28  Kisha wakaondoka Tera na kupiga kambi Mithka. 29  Baadaye wakaondoka Mithka na kupiga kambi Hashmona. 30  Kisha wakaondoka Hashmona na kupiga kambi Moserothi. 31  Halafu wakaondoka Moserothi na kupiga kambi Bene-yaakani.+ 32  Kisha wakaondoka Bene-yaakani na kupiga kambi Hor-hagidgadi. 33  Halafu wakaondoka Hor-hagidgadi na kupiga kambi Yotbata.+ 34  Baadaye wakaondoka Yotbata na kupiga kambi Abrona. 35  Kisha wakaondoka Abrona na kupiga kambi Esion-geberi.+ 36  Kisha wakaondoka Esion-geberi na kupiga kambi katika nyika ya Zini,+ yaani, Kadeshi. 37  Baadaye wakaondoka Kadeshi na kupiga kambi kwenye Mlima Hori,+ mpakani mwa nchi ya Edomu. 38  Kisha kuhani Haruni akapanda juu ya Mlima Hori kwa agizo la Yehova, akafa huko siku ya kwanza ya mwezi wa tano, mwaka wa 40 tangu Waisraeli walipotoka nchini Misri.+ 39  Haruni alikuwa na umri wa miaka 123 alipokufa juu ya Mlima Hori. 40  Basi mfalme wa Aradi,+ Mkanaani, aliyekuwa akiishi Negebu katika nchi ya Kanaani, akasikia kwamba Waisraeli wanakuja. 41  Baada ya muda wakaondoka kwenye Mlima Hori+ na kupiga kambi Salmona. 42  Kisha wakaondoka Salmona na kupiga kambi Punoni. 43  Halafu wakaondoka Punoni na kupiga kambi Obothi.+ 44  Wakaondoka Obothi na kupiga kambi Iye-abarimu kwenye mpaka wa Moabu.+ 45  Baadaye wakaondoka Iyimu* na kupiga kambi Dibon-gadi.+ 46  Kisha wakaondoka Dibon-gadi na kupiga kambi Almon-diblathaimu. 47  Halafu wakaondoka Almon-diblathaimu na kupiga kambi kwenye milima ya Abarimu+ karibu na Nebo.+ 48  Mwishowe wakaondoka kwenye milima ya Abarimu na kupiga kambi katika jangwa tambarare la Moabu karibu na Yordani huko Yeriko.+ 49  Wakaendelea kupiga kambi kandokando ya Mto Yordani kuanzia Beth-yeshimothi mpaka Abel-shitimu,+ katika jangwa tambarare la Moabu. 50  Yehova akazungumza na Musa katika jangwa tambarare la Moabu karibu na Yordani huko Yeriko, akamwambia: 51  “Waambie hivi Waisraeli: ‘Mnavuka Mto Yordani kuingia katika nchi ya Kanaani.+ 52  Ni lazima muwafukuze wakaaji wote wa nchi hiyo kutoka mbele yenu na kuharibu sanamu zao zote za mawe+ na sanamu zao zote za chuma,*+ nanyi mnapaswa kuharibu mahali pao pote patakatifu palipo juu.+ 53  Mtaimiliki nchi hiyo na kuishi humo, kwa maana hakika nitawapa nchi hiyo ili mwimiliki.+ 54  Mtaigawanya nchi hiyo kwa kura+ na kuimiliki kulingana na familia zenu. Kundi kubwa litapokea urithi mkubwa zaidi na kikundi kidogo kitapokea urithi mdogo.+ Kila mtu atapokea urithi wake mahali ambapo kura yake itaangukia. Mtapokea urithi wenu wa nchi kulingana na makabila ya baba zenu.+ 55  “‘Hata hivyo, msipowafukuza wakaaji wa nchi hiyo kutoka mbele yenu,+ basi wale mtakaoruhusu wabaki watakuwa kama vibanzi katika macho yenu na kama miiba kwenye mbavu zenu, nao watawasumbua katika nchi mtakayoishi.+ 56  Nami nitawatendea ninyi mambo niliyokusudia kuwatendea wao.’”+

Maelezo ya Chini

Tnn., “majeshi yao.”
Tnn., “mkono ulioinuliwa.”
Huu ni ufupisho wa Iye-abarimu.
Tnn., “za kuyeyushwa.”