Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Kitabu cha Pili cha Samweli

Sura

Muhtasari wa Yaliyomo

 • 1

  • Daudi apata habari za kifo cha Sauli (1-16)

  • Daudi aimba wimbo wa kumwombolezea Sauli na Yonathani (17-27)

 • 2

  • Daudi, mfalme wa Yuda (1-7)

  • Ish-boshethi, mfalme wa Israeli (8-11)

  • Vita kati ya nyumba ya Daudi na nyumba ya Sauli (12-32)

 • 3

  • Nyumba ya Daudi yazidi kupata nguvu (1)

  • Wana wa Daudi (2-5)

  • Abneri ajiunga na Daudi (6-21)

  • Yoabu amuua Abneri (22-30)

  • Daudi amwombolezea Abneri (31-39)

 • 4

  • Ish-boshethi auawa (1-8)

  • Daudi aagiza waliomuua Ish-boshethi wauawe (9-12)

 • 5

  • Daudi awekwa kuwa mfalme wa nchi yote ya Israeli (1-5)

  • Yerusalemu latekwa (6-16)

   • Sayuni, Jiji la Daudi (7)

  • Daudi awashinda Wafilisti (17-25)

 • 6

  • Sanduku la agano laletwa Yerusalemu (1-23)

   • Uza alikamata sanduku la agano na kuuawa (6-8)

   • Mikali amdharau Daudi (16, 20-23)

 • 7

  • Daudi hatajenga hekalu (1-7)

  • Agano pamoja na Daudi kwa ajili ya ufalme (8-17)

  • Sala ya Daudi ya shukrani (18-29)

 • 8

  • Ushindi mbalimbali wa Daudi (1-14)

  • Wakuu katika utawala wa Daudi (15-18)

 • 9

  • Daudi amtendea Mefiboshethi kwa upendo mshikamanifu (1-13)

 • 10

  • Awashinda Waamoni na Wasiria (1-19)

 • 11

  • Daudi afanya uzinzi na Bath-sheba (1-13)

  • Daudi apanga Uria auawe (14-25)

  • Daudi amchukua Bath-sheba kuwa mke wake (26, 27)

 • 12

  • Nathani amkaripia Daudi (1-15a)

  • Mwana wa Bath-sheba afa (15b-23)

  • Bath-sheba amzaa Sulemani (24, 25)

  • Jiji la Raba la Waamoni latekwa (26-31)

 • 13

  • Amnoni ambaka Tamari (1-22)

  • Absalomu amuua Amnoni (23-33)

  • Absalomu akimbilia Geshuri (34-39)

 • 14

  • Yoabu na mwanamke Mtekoa (1-17)

  • Daudi agundua njama ya Yoabu (18-20)

  • Absalomu aruhusiwa kurudi (21-33)

 • 15

  • Njama na uasi wa Absalomu (1-12)

  • Daudi akimbia kutoka Yerusalemu (13-30)

  • Ahithofeli ajiunga na Absalomu (31)

  • Hushai atumwa kuvuruga ushauri wa Ahithofeli (32-37)

 • 16

  • Siba amchongea Mefiboshethi (1-4)

  • Shimei amtukana Daudi (5-14)

  • Absalomu ampokea Hushai (15-19)

  • Ushauri wa Ahithofeli (20-23)

 • 17

  • Hushai avuruga ushauri wa Ahithofeli (1-14)

  • Daudi aonywa; amtoroka Absalomu (15-29)

   • Barzilai na wengine wamletea vyakula (27-29)

 • 18

  • Absalomu ashindwa; kifo chake (1-18)

  • Daudi ajulishwa kuhusu kifo cha Absalomu (19-33)

 • 19

  • Daudi amwombolezea Absalomu (1-4)

  • Yoabu amkaripia Daudi (5-8a)

  • Daudi arudi Yerusalemu (8b-15)

  • Shimei aomba msamaha (16-23)

  • Mefiboshethi athibitishwa kuwa hana hatia (24-30)

  • Barzilai aheshimiwa (31-40)

  • Makabila yazozana (41-43)

 • 20

  • Uasi wa Sheba; Yoabu amuua Amasa (1-13)

  • Sheba afuatwa na kukatwa kichwa (14-22)

  • Wakuu katika utawala wa Daudi (23-26)

 • 21

  • Nyumba ya Sauli yalipizwa kisasi kwa ajili ya Wagibeoni (1-14)

  • Vita dhidi ya Wafilisti (15-22)

 • 22

  • Daudi amsifu Mungu kwa sababu ya matendo yake ya wokovu (1-51)

   • “Yehova ni jabali langu” (2)

   • Yehova ni mshikamanifu kwa walio washikamanifu (26)

 • 23

  • Maneno ya mwisho ya Daudi (1-7)

  • Mambo yaliyotendwa na mashujaa hodari wa Daudi (8-39)

 • 24

  • Dhambi ya Daudi ya kuwahesabu watu (1-14)

  • Ugonjwa hatari wasababisha vifo vya watu 70,000 (15-17)

  • Daudi ajenga madhabahu (18-25)

   • Hatatoa dhabihu ambazo hazimgharimu (24)