Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Kitabu cha Ezekieli

Sura

Muhtasari wa Yaliyomo

 • 1

  • Ezekieli aona maono ya Mungu akiwa Babiloni (1-3)

  • Maono ya gari la kimbingu la Yehova (4-28)

   • Dhoruba, wingu, na moto (4)

   • Viumbe hai wanne (5-14)

   • Magurudumu manne (15-21)

   • Anga linalometameta kama barafu (22-24)

   • Kiti cha ufalme cha Yehova (25-28)

 • 2

  • Ezekieli apewa kazi ya kuwa nabii (1-10)

   • ‘Iwe watasikiliza au hawatasikiliza’ (5)

   • Aonyeshwa kitabu cha kukunjwa chenye nyimbo za huzuni (9, 10)

 • 3

  • Ezekieli aambiwa ale kitabu cha kukunjwa alichopewa na Mungu (1-15)

  • Ezekieli atakuwa mlinzi (16-27)

   • Kupuuza kunasababisha hatia ya damu (18-21)

 • 4

  • Aonyesha jinsi Yerusalemu litakavyozingirwa (1-17)

   • Abeba hatia kwa siku 390 na siku 40 (4-7)

 • 5

  • Aonyesha jinsi Yerusalemu litakavyoanguka (1-17)

   • Nywele za nabii zilizonyolewa zagawanywa katika mafungu matatu (1-4)

   • Yerusalemu lina uovu kuliko mataifa (7-9)

   • Waasi waadhibiwa kwa njia tatu (12)

 • 6

  • Dhidi ya milima ya Israeli (1-14)

   • Sanamu zinazochukiza zitafedheheshwa (4-6)

   • “Mtalazimika kujua kwamba mimi ni Yehova” (7)

 • 7

  • Mwisho umefika (1-27)

   • Msiba wa pekee (5)

   • Pesa zatupwa barabarani (19)

   • Hekalu litatiwa unajisi (22)

 • 8

  • Ezekieli apelekwa Yerusalemu katika maono (1-4)

  • Vitu vinavyochukiza vyaonekana hekaluni (5-18)

   • Wanawake wakimlilia Tamuzi (14)

   • Wanaume wakiabudu jua (16)

 • 9

  • Wanaume sita wanaoangamiza na mwanamume mwenye kidau cha wino (1-11)

   • Hukumu itaanzia patakatifu (6)

 • 10

  • Moto wachukuliwa kutoka kati ya magurudumu (1-8)

  • Ufafanuzi kuhusu makerubi na magurudumu (9-17)

  • Utukufu wa Mungu waondoka hekaluni (18-22)

 • 11

  • Wakuu waovu washutumiwa (1-13)

   • Jiji lafananishwa na chungu cha kupikia (3-12)

  • Ahadi ya kurudishwa (14-21)

   • Wapewa “roho mpya” (19)

  • Utukufu wa Yehova waondoka Yerusalemu (22, 23)

  • Ezekieli arudi Ukaldayo katika maono (24, 25)

 • 12

  • Atabiri uhamisho kwa mifano (1-20)

   • Mizigo ya kwenda uhamishoni (1-7)

   • Mkuu ataondoka kukiwa na giza (8-16)

   • Mkate wa wasiwasi, maji ya hofu (17-20)

  • Msemo wa udanganyifu wathibitika kuwa uwongo (21-28)

   • “Hakuna neno langu lolote litakalokawia” (28)

 • 13

  • Dhidi ya manabii wa uwongo (1-16)

   • Kuta zilizopakwa chokaa zitaanguka (10-12)

  • Dhidi ya manabii wa kike wa uwongo (17-23)

 • 14

  • Wanaoabudu sanamu washutumiwa (1-11)

  • Hukumu dhidi ya Yerusalemu haiwezi kuepukika (12-23)

   • Noa, Danieli, na Ayubu waliokuwa waadilifu (14, 20)

 • 15

  • Yerusalemu, mzabibu usiofaa (1-8)

 • 16

  • Upendo wa Mungu kwa Yerusalemu (1-63)

   • Apatikana kama mtoto aliyeachwa (1-7)

   • Mungu ampamba na kufanya agano la ndoa pamoja naye (8-14)

   • Akosa kuwa mwaminifu (15-34)

   • Aadhibiwa kama mwanamke mzinzi (35-43)

   • Alinganishwa na Samaria na Sodoma (44-58)

   • Mungu akumbuka agano lake (59-63)

 • 17

  • Kitendawili cha tai wawili na mzabibu (1-21)

  • Chipukizi changa litakuwa mwerezi mkubwa (22-24)

 • 18

  • Kila mtu anawajibika kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe (1-32)

   • Nafsi inayotenda dhambi itakufa (4)

   • Mwana hatalipia dhambi ya baba yake (19, 20)

   • Sifurahishwi na kifo cha mtu mwovu (23)

   • Toba huhifadhi uhai (27, 28)

 • 19

  • Wimbo wa huzuni kwa ajili ya wakuu wa Israeli (1-14)

 • 20

  • Historia ya uasi wa Waisraeli (1-32)

  • Ahadi ya kurudishwa kwa Waisraeli (33-44)

  • Unabii dhidi ya kusini (45-49)

 • 21

  • Upanga wa hukumu wa Mungu wachomolewa (1-17)

  • Mfalme wa Babiloni kushambulia Yerusalemu (18-24)

  • Mkuu mwovu wa Israeli ataondolewa (25-27)

   • “Ulivue taji” (26)

   • “Mpaka yule aliye na haki ya kisheria atakapokuja” (27)

  • Upanga utawashambulia Waamoni (28-32)

 • 22

  • Yerusalemu, jiji lenye hatia ya damu (1-16)

  • Waisraeli ni kama takataka isiyo na thamani (17-22)

  • Viongozi na watu wa Israeli washutumiwa (23-31)

 • 23

  • Dada wawili ambao si waaminifu (1-49)

   • Ohola na Ashuru (5-10)

   • Oholiba na Babiloni na Misri (11-35)

   • Kuadhibiwa kwa dada wawili (36-49)

 • 24

  • Yerusalemu kama chungu cha kupikia chenye kutu (1-14)

  • Kifo cha mke wa Ezekieli ni ishara (15-27)

 • 25

  • Unabii dhidi ya Amoni (1-7)

  • Unabii dhidi ya Moabu (8-11)

  • Unabii dhidi ya Edomu (12-14)

  • Unabii dhidi ya Ufilisti (15-17)

 • 26

  • Unabii dhidi ya Tiro (1-21)

   • “Uwanja wa kukaushia nyavu za kukokotwa” (5, 14)

   • Mawe na udongo vyatupwa ndani ya maji (12)

 • 27

  • Wimbo wa huzuni kuhusu meli inayozama ya Tiro (1-36)

 • 28

  • Unabii dhidi ya mfalme wa Tiro (1-10)

   • “Mimi ni mungu” (2, 9)

  • Wimbo wa huzuni kuhusu mfalme wa Tiro (11-19)

   • “Ulikuwa katika Edeni” (13)

   • “Kerubi anayefunika aliyetiwa mafuta” (14)

   • ‘Uovu ulipatikana ndani yako’ (15)

  • Unabii dhidi ya Sidoni (20-24)

  • Israeli watarudishwa (25, 26)

 • 29

  • Unabii dhidi ya Farao (1-16)

  • Jiji la Babiloni litapewa Misri kama malipo (17-21)

 • 30

  • Unabii dhidi ya Misri (1-19)

   • Shambulizi la Nebukadneza latabiriwa (10)

  • Nguvu za Farao zavunjwa (20-26)

 • 31

  • Kuanguka kwa Misri, mwerezi mrefu (1-18)

 • 32

  • Wimbo wa huzuni kuhusu Farao na Misri (1-16)

  • Misri kuzikwa pamoja na wasiotahiriwa (17-32)

 • 33

  • Majukumu ya mlinzi (1-20)

  • Habari kuhusu kuanguka kwa Yerusalemu (21, 22)

  • Ujumbe kwa wakaaji wa magofu ya Yerusalemu (23-29)

  • Watu wapuuza ujumbe (30-33)

   • Ezekieli “kama wimbo wa mapenzi” (32)

   • “Nabii alikuwa miongoni mwao” (33)

 • 34

  • Unabii dhidi ya wachungaji wa Israeli (1-10)

  • Jinsi Yehova anavyowatunza kondoo wake (11-31)

   • “Mtumishi wangu Daudi” atawachunga (23)

   • “Agano la amani” (25)

 • 35

  • Unabii dhidi ya milima ya Seiri (1-15)

 • 36

  • Unabii kuhusu milima ya Israeli (1-15)

  • Kurudishwa kwa Waisraeli (16-38)

   • “Nitalitakasa jina langu kuu” (23)

   • “Kama bustani ya Edeni” (35)

 • 37

  • Maono ya bonde la mifupa mikavu (1-14)

  • Vijiti viwili vitaunganishwa pamoja (15-28)

   • Taifa moja chini ya mfalme mmoja (22)

   • Agano la kudumu la amani (26)

 • 38

  • Gogu kushambulia Israeli (1-16)

  • Hasira ya Yehova dhidi ya Gogu (17-23)

   • ‘Mataifa yatalazimika kujua kwamba mimi ni Yehova’ (23)

 • 39

  • Kuangamizwa kwa Gogu na vikosi vyake (1-10)

  • Mazishi katika Bonde la Hamoni-Gogu (11-20)

  • Kurudishwa kwa Waisraeli (21-29)

   • Roho ya Mungu yamiminwa juu ya Waisraeli (29)

 • 40

  • Ezekieli aletwa Israeli katika maono (1, 2)

  • Ezekieli aona hekalu kwenye maono (3, 4)

  • Nyua na malango (5-47)

   • Lango la nje la mashariki (6-16)

   • Ua wa nje; malango mengine (17-26)

   • Ua wa ndani na malango (27-37)

   • Vyumba vya utumishi wa hekaluni (38-46)

   • Madhabahu (47)

  • Ukumbi wa hekalu (48, 49)

 • 41

  • Patakatifu pa hekalu (1-4)

  • Ukuta na vyumba vya kando (5-11)

  • Jengo la magharibi (12)

  • Majengo yapimwa (13-15a)

  • Sehemu ya ndani ya patakatifu (15b-26)

 • 42

  • Majengo ya vyumba vya kulia chakula (1-14)

  • Pande nne za hekalu zapimwa (15-20)

 • 43

  • Utukufu wa Yehova wajaa hekaluni (1-12)

  • Madhabahu (13-27)

 • 44

  • Lango la mashariki kubaki likiwa limefungwa (1-3)

  • Maagizo kuhusu wageni (4-9)

  • Maagizo kwa ajili ya Walawi na makuhani (10-31)

 • 45

  • Mchango mtakatifu na jiji (1-6)

  • Sehemu ya kiongozi (7, 8)

  • Viongozi watatenda kwa unyoofu (9-12)

  • Michango ya watu na ya kiongozi (13-25)

 • 46

  • Matoleo ya pindi mbalimbali (1-15)

  • Kurithi mali ya kiongozi (16-18)

  • Sehemu za kuchemshia dhabihu (19-24)

 • 47

  • Kijito kinachotiririka kutoka hekaluni (1-12)

   • Kina cha maji chaongezeka hatua kwa hatua (2-5)

   • Maji ya Bahari ya Chumvi yaponywa (8-10)

   • Sehemu zenye majimaji haziponywi (11)

   • Miti kwa ajili ya chakula na kuponya (12)

  • Mipaka ya nchi (13-23)

 • 48

  • Kuigawa nchi (1-29)

  • Malango 12 ya jiji (30-35)

   • Jiji linaloitwa “Yehova Yupo Hapo” (35)