Ayubu 13:1-28

13  “Tazama! Jicho langu limeona hayo yote,Sikio langu limesikia nalo linayafikiria.   Mambo ambayo ninyi mnajua hata mimi nayajua vema pia;Mimi si mdogo kuliko ninyi.+   Hata hivyo mimi, kwa upande wangu, ningesema na Mweza-Yote mwenyewe,+Nami ningependezwa kuhojiana na Mungu.   Kwa upande mwingine, ninyi ni watu wa kupaka uwongo;+Ninyi nyote ni matabibu wasio na faida.+   Laiti mngenyamaza kabisa,Ili iwe hekima kwa upande wenu!+   Tafadhali, sikieni hoja zangu za kujibu,+Na msikilize kwa makini maombi ya midomo yangu.   Je, ninyi mtasema maneno ya ukosefu wa uadilifu kwa ajili ya Mungu mwenyewe,Na je, mtasema udanganyifu kwa ajili yake?+   Je, mtamtendea kwa upendeleo,+Au, je, kwa ajili ya Mungu wa kweli mtashindana katika kesi?   Je, ingekuwa vema kwamba awachunguze ninyi?+Au, je, mtacheza na yeye kama mtu anavyocheza na mwanadamu anayeweza kufa? 10  Hakika atawakaripia ninyi+Ikiwa mnajaribu kuonyesha ubaguzi kisiri;+ 11  Je, utukufu wake hautawafanya mshtuke kwa woga,Na hofu yake ianguke juu yenu?+ 12  Maneno yenu ya kukumbukwa ni methali za majivu;Vinundu vya ngao zenu ni kama vinundu vya ngao vya udongo.+ 13  Nyamazeni mbele yangu, ili mimi mwenyewe nipate kusema.Kisha na lije juu yangu jambo lolote lile! 14  Kwa nini ninabeba nyama ya mwili wangu katika meno yanguNa kutia nafsi yangu mwenyewe mkononi mwangu?+ 15  Hata kama angeniua, je, singengojea?+Ningetoa hoja tu usoni pake kwa ajili ya njia zangu. 16  Yeye pia angekuwa wokovu wangu,+Kwa maana hakuna mwasi-imani yeyote atakayekuja mbele zake.+ 17  Sikieni neno langu kabisa,+Na tangazo langu liwe masikioni mwenu. 18  Tazama! Tafadhali, nimeleta kesi ya haki;+Ninajua vema kwamba mimi mwenyewe niko upande wa haki. 19  Ni nani atakayeshindana na mimi?+Kwa maana sasa kama ningenyamaza kimya ningekata pumzi tu! 20  Ila tu usinitendee mambo mawili;Hapo basi sitajificha kwa sababu yako tu;+ 21  Ondoa mkono wako mbali sana kutoka juu yangu,Na hofu kutoka kwako—isinitie woga.+ 22  Ama uite ili mimi mwenyewe nijibu;Au mimi niseme, nawe unipe jibu. 23  Mimi nina makosa na dhambi kwa njia gani?Nijulishe maasi yangu na dhambi yangu. 24  Kwa nini unaficha uso wako+Na kuniona mimi kama adui yako?+ 25  Je, utafanya jani linalopeperushwa litetemeke,Au kuendelea kuyafukuza majani makavu tu? 26  Kwa maana unaendelea kuandika juu yangu mambo machungu+Nawe unanifanya niyapate matokeo ya makosa ya ujana wangu.+ 27  Pia unaendelea kuiweka miguu yangu katika mikatale,+Nawe unaziangalia njia zangu zote;Unatia alama ya mstari wako kwa ajili ya nyayo za miguu yangu. 28  Naye ni kama kitu kilichooza ambacho huchakaa;+Kama vazi ambalo nondo kweli hula.+

Maelezo ya Chini