Ayubu 28:1-28

28  “Kwa kweli, kuna mahali pa kupata fedhaNa mahali pa dhahabu ambayo wanasafisha;+   Chuma hutolewa katika mavumbi+Na shaba humwagwa kutoka katika mawe.   Ameweka mwisho wa giza;Naye hutafuta mipaka yote+Jiwe katika giza na kivuli kizito.   Amechimba shimo mbali sana na mahali ambapo watu hukaa ugenini,+Mahali paliposahauliwa, mbali na mguu;Baadhi ya wanadamu wanaoweza kufa wameshuka chini, wamening’inia.   Kwa habari ya dunia, chakula hutoka humo;+Lakini chini yake, imepinduliwa kana kwamba ni kwa moto.   Mawe yake ni mahali pa yakuti,+Nayo ina vumbi la dhahabu.   Njia—hakuna ndege mwenye kuwinda+ ambaye ameijua,Wala jicho la mwewe mweusi+ halikuiona.   Wanyama wa mwituni wenye fahari hawajaikanyaga ikawa ngumu;Mwana-simba hakutembea juu yake.   Ametia mkono wake juu ya jiwe gumu;Ameipindua milima kutoka katika mizizi yake; 10  Amechimba ndani ya miamba mifereji iliyojaa maji,+Na jicho lake limeona vitu vyote vyenye thamani. 11  Ametengeneza bwawa mahali ambapo mito ilitiririka,+Naye hukileta katika nuru kitu kilichofichwa. 12  Lakini hekima—inaweza kupatikana wapi,+Na sasa, pako wapi mahali pa uelewaji? 13  Mwanadamu anayeweza kufa hajajua thamani yake,+Nayo haipatikani katika nchi ya walio hai. 14  Kilindi cha maji kimesema,‘Haimo ndani yangu!’Bahari pia imesema, ‘Haipo pamoja nami!’+ 15  Dhahabu safi haiwezi kubadilishwa nayo,+Wala fedha haiwezi kupimwa kuwa bei yake. 16  Haiwezi kulipiwa kwa dhahabu ya Ofiri,+Wala kwa jiwe la shohamu lisilopatikana kwa urahisi wala yakuti. 17  Dhahabu na kioo haviwezi kulinganishwa nayo,Wala chombo chochote cha dhahabu safi hakiwezi kubadilishwa nayo. 18  Marijani+ na fuwele ya mawe havitatajwa,Bali mfuko uliojaa hekima ni wenye thamani kuliko ule uliojaa lulu.+ 19  Topazi+ ya Kushi haiwezi kulinganishwa nayo;Haiwezi kulipiwa hata kwa dhahabu safi. 20  Lakini hekima—hiyo inatoka wapi,+Na sasa, pako wapi mahali pa uelewaji? 21  Imefichwa kutoka machoni pa kila mtu aliye hai,+Nayo imefichwa kutoka kwa viumbe vinavyoruka vya mbinguni. 22  Maangamizi na kifo zimesema,‘Tumesikia habari zake kwa masikio yetu.’ 23  Mungu, Yeye ndiye ameelewa njia yake,+Naye mwenyewe amejua mahali pake, 24  Kwa maana yeye anatazama mpaka miisho ya dunia;+Anaona chini ya mbingu zote, 25  Ili kuupima upepo,+Naye ameyapima maji kwa kipimo;+ 26  Alipofanyiza sharti kwa ajili ya mvua,+Na njia kwa ajili ya wingu la dhoruba lenye kunguruma, 27  Ndipo alipoiona hekima kisha akasema habari zake;Aliitayarisha na pia akaichunguza kabisa. 28  Naye akamwambia mwanadamu,‘Tazama! Kumwogopa Yehova—hiyo ndiyo hekima,+Na kuacha ubaya ni uelewaji.’”+

Maelezo ya Chini