Ayubu 19:1-29

19  Naye Ayubu akajibu, akasema:   “Ninyi mtaendelea kunikasirisha nafsi yangu mpaka wakati gani+Na kuendelea kuniponda kwa maneno?+   Hizi mara kumi mmenikemea;Hamna aibu kwamba mnanitendea kwa ugumu hivyo.+   Na, kama nimefanya kosa,+Hilo kosa litakaa pamoja nami.   Ikiwa kwa kweli mnajivuna sana juu yangu,+Na kuonyesha kwamba shutuma yangu inanifaa,+   Jueni, basi, kwamba Mungu mwenyewe amenipotosha,Naye ameuzungusha wavu wake wa kuwindia juu yangu.+   Tazama! Ninaendelea kupaaza sauti, ‘Jeuri!’ lakini sipati jibu lolote;+Naendelea kulia nipewe msaada, lakini hakuna haki.+   Amezuia pito langu kwa ukuta wa mawe,+ nami siwezi kupita;Naye anaweka giza katika barabara zangu.+   Amenivua utukufu wangu,+Naye anaondoa taji la kichwa changu. 10  Ananibomoa pande zote, nami naenda zangu;Naye anang’oa tumaini langu kama mti. 11  Pia hasira yake inawaka juu yangu,+Naye anaendelea kunihesabu kuwa adui yake. 12  Vikosi vyake vinakuja kwa muungano na kujenga njia yao juu yangu,+Nao wanapiga kambi kuzunguka hema langu. 13  Ndugu zangu amewaweka mbali sana nami,+Na wale wanaonijua hata wamejitenga nami. 14  Watu ninaofahamiana nao wamekoma kuwapo,+Na wale ninaowajua wamenisahau, 15  Wale wanaokaa wakiwa wageni nyumbani mwangu;+ na vijakazi wangu wananiona kuwa mgeni;Nimekuwa mgeni kwelikweli machoni pao. 16  Nimemwita mtumishi wangu, lakini hajibu.Ninaendelea kumwomba huruma kwa kinywa changu mwenyewe. 17  Pumzi yangu imemchukiza mke wangu,+Nami nimenuka kwa wana wa tumbo la mama yangu. 18  Pia wavulana wadogo wenyewe wamenikataa;+Ninaposimama tu, wanaanza kunisema. 19  Watu wote wa kikundi cha rafiki zangu wananichukia,+Na wale ambao nimewapenda wamenigeuka.+ 20  Mifupa yangu inashikamana na ngozi na nyama yangu,+Nami ninaponyoka na ngozi ya meno yangu. 21  Mnionyeshe kibali kidogo, mnionyeshe kibali kidogo, enyi rafiki zangu,+Kwa kuwa mkono wenyewe wa Mungu umenigusa.+ 22  Kwa nini mnaendelea kunitesa kama anavyofanya Mungu,+Na hamshibi nyama yangu? 23  Laiti sasa maneno yangu yangekuwa yameandikwa!Laiti yangekuwa yameandikwa katika kitabu! 24  Kwa kalamu ya chuma+ na kwa risasi,Laiti yangekuwa yamechongwa milele katika mwamba! 25  Nami mwenyewe najua vema kwamba mkombozi wangu+ yuko hai,Na kwamba, akija baada yangu, yeye atasimama+ juu ya mavumbi. 26  Na baada ya ngozi yangu, ambayo wameichuna,—hii!Lakini ijapokuwa kupungua kwa mwili wangu nitamwona Mungu, 27  Ambaye mimi mwenyewe nitamwona,+Na ambaye macho yangu hakika yatamwona, bali si mgeni.Figo zangu zimeisha nguvu ndani yangu kabisa. 28  Kwa maana ninyi mnasema, ‘Kwa nini tunaendelea kumtesa?’+Wakati mzizi wenyewe wa jambo hili unapatikana ndani yangu. 29  Ogopeni kwa ajili yenu kwa sababu ya upanga,+Kwa kuwa upanga unamaanisha ghadhabu juu ya makosa,Ili ninyi mjue kwamba kuna mwamuzi.”+

Maelezo ya Chini