Ayubu 4:1-21

4  Naye Elifazi+ Mtemani akajibu, akasema:   “Mtu akijaribu kusema nawe, je, utachoka?Lakini ni nani anayeweza kuzuia maneno?   Tazama! Umewarekebisha wengi,+Nawe ulikuwa ukiitia nguvu+ mikono iliyo dhaifu.   Maneno yako yalimwinua mtu yeyote mwenye kujikwaa;+Nawe uliyaimarisha magoti yanayoyumba-yumba.+   Lakini wakati huu yanakupata wewe, nawe unachoka;Yanakugusa wewe, nawe unaingiwa na wasiwasi.   Je, heshima yako kwa Mungu siyo msingi wa uhakika wako?Je, tumaini lako silo utimilifu+ wa njia zako?   Tafadhali, kumbuka hili: Je, ni nani aliyepata kuangamia bila hatia?Na wanyoofu+ walipata kufutiliwa mbali wapi?   Kulingana na yale ambayo nimeona, wale wanaotunga madharaNa wale wanaopanda taabu wataivuna wenyewe.+   Wao huangamia kupitia pumzi ya Mungu,Nao hufikia mwisho kupitia roho ya hasira yake. 10  Kuna mngurumo wa simba, na sauti ya mwana-simba,Lakini meno ya wana-simba wenye manyoya shingoni huvunjika. 11  Simba anaangamia kwa kukosa mawindo,Na watoto wa simba hutenganishwa. 12  Sasa mimi nililetewa neno kwa siri,Na sikio langu likasikia mnong’ono wake,+ 13  Katika fikira zinazofadhaisha kutokana na maono ya usiku,Wakati usingizi mzito unapowashika wanadamu. 14  Hofu ilinishika, na kutetemeka,Nayo ikaijaza hofu mifupa yangu iliyo mingi. 15  Na roho fulani ikapita juu ya uso wangu;Nywele za mwili wangu zikaanza kusimama. 16  Ikaanza kusimama tuli,Lakini sikuitambua sura yake;Umbo fulani lilikuwa mbele ya macho yangu;Kulikuwa na utulivu, na sasa nikasikia sauti: 17  ‘Mwanadamu anayeweza kufa—je, anaweza kuwa mwenye haki kuliko Mungu mwenyewe?Au, je, mwanamume anaweza kuwa safi kuliko Mtengenezaji wake mwenyewe?’ 18  Tazama! Yeye hana imani katika watumishi wake,Naye huwashtaki wajumbe wake kuwa na makosa. 19  Sembuse wale wanaokaa katika nyumba za udongo,Ambao msingi wao umo mavumbini!+Mtu huwaponda upesi kuliko nondo. 20  Kuanzia asubuhi mpaka jioni wao hupondwa vipande-vipande;Wao huangamia milele bila yeyote kutia hilo moyoni. 21  Je, kamba yao ya hema iliyo ndani yao haikung’olewa?Wao hufa kwa kukosa hekima.

Maelezo ya Chini