Ayubu 30:1-31
30 “Na sasa wamenicheka,+Wale wenye siku chache kuliko mimi,+Ambao baba zao ningekataaKuwaweka pamoja na mbwa wa kundi langu.
2 Hata nguvu za mikono yao—zilinifaa nini?Nguvu zimekwisha ndani yao.+
3 Wao ni tasa kwa sababu ya upungufu na njaa,Wanatafuna eneo lisilo na maji,+Ambapo jana palikuwa na dhoruba na ukiwa.
4 Walikuwa waking’oa mmea wa chumvi kando ya vichaka,Na mzizi wa miretemu ulikuwa chakula chao.
5 Walikuwa wakifukuzwa kutoka katika jamii;+Watu waliwapaazia sauti kama kupaazia mwizi.
6 Wanalazimika kukaa kwenye mteremko wa mabonde ya mito,Katika matundu ya mavumbi na katika miamba.
7 Walilia katikati ya vichaka;Walisongamana pamoja chini ya upupu.
8 Wana wa mtu asiye na akili,+ pia wana wa mtu asiye na jina,Wamepigwa mijeledi watoke katika nchi.
9 Na sasa mimi nimekuwa hata kichwa cha wimbo wao,+Nami ni simango kwao.+
10 Wamenichukia, wamekaa mbali nami;+Nao hawakuacha kunitemea mate usoni.+
11 Kwa kuwa aliifungua kamba yangu ya upinde na kuninyenyekeza,Nao waliifungua lijamu kwa sababu yangu.
12 Wanasimama upande wa mkono wangu wa kuume kama kundi la waovu;Wameachilia miguu yangu,Lakini wakajenga juu yangu vizuizi vyao vyenye kuleta msiba.+
13 Wameziharibu barabara zangu;Walizidisha shida kwangu,+Bila wao kuwa na msaidizi yeyote.
14 Walikuja kana kwamba ni kupitia pengo pana;Wamejiviringisha katika dhoruba.
15 Vitisho vya ghafula vimegeuzwa juu yangu;Cheo changu cha heshima kinafukuzwa kama upepo,Na wokovu wangu umepitilia mbali kama wingu.
16 Na sasa nafsi yangu inamwagwa ndani yangu;+Siku za mateso+ zinanishika.
17 Mifupa+ yangu imetobolewa usiku na kuanguka kutoka kwangu,Na maumivu yanayonitafuna hayapumziki.+
18 Vazi langu linabadilika kutokana na wingi wa nguvu;Linanifunga kama ukosi wa vazi langu refu.
19 Amenishusha chini katika udongo,Hivi kwamba nimekuwa kama mavumbi na majivu.
20 Ninakulilia nipate msaada, lakini wewe hunijibu;+Nimesimama, ili unikazie fikira.
21 Unajibadili ili uwe mkatili kwangu;+Unadumisha uadui kwangu kwa nguvu kamili za mkono wako.
22 Unaniinua kwenye upepo, unanifanya niupande;Kisha unaniyeyusha kwa kishindo.
23 Kwa maana najua vema kwamba utanirudisha kwenye kifo,+Na kwenye nyumba ya kukutania ya kila mtu aliye hai.
24 Ila tu hakuna yeyote anayeunyoosha mkono wake juu ya rundo la mabomoko matupu,+Wala wakati wa kudhoofika kwa mtu hakuna kilio cha kuomba msaada kuhusu mambo hayo.
25 Hakika nimemlilia mtu aliye na siku ngumu;+Nafsi yangu imemhuzunikia maskini.+
26 Ijapokuwa nilingojea mema, mabaya yalikuja;+Nami nikaendelea kungojea nuru, lakini giza likaja.
27 Matumbo yangu yalichemshwa wala hayakukaa kimya;Siku za mateso zilinikabili.
28 Nilitembea huku na huku kwa huzuni+ wakati ambapo hakukuwa nuru ya jua;Nilisimama katika kutaniko, nikaendelea kulia nipewe msaada.
29 Nikawa ndugu ya mbwa-mwitu,Na rafiki ya binti za mbuni.+
30 Ngozi yangu ikawa nyeusi+ na kuanguka kutoka kwangu,Na mifupa yangu ikawaka moto kutokana na ukavu.
31 Na kinubi changu kikawa cha maombolezo matupu,Na zumari yangu kwa ajili ya sauti ya watu wanaolia.

