Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

JW BROADCASTING

Sakinisha Programu ya JW Broadcasting Kwenye Amazon Fire TV

Sakinisha Programu ya JW Broadcasting Kwenye Amazon Fire TV

Ili kutazama JW Broadcasting kupitia Amazon Fire TV, unahitaji kusakinisha programu ya JW Broadcasting kwenye Fire TV. Fuata hatua zifuatazo:

 Unganisha Amazon Fire TV

Amazon Fire TV ina miongozo ambayo inaweza kukusaidia kuitumia na kuunganishwa kwenye intaneti. Baada ya kuunganisha Amazon Fire TV, malizia kwa kufuata maagizo yaliyoandikwa kwenye skrini. Unaweza kupata ujumbe wa kuombwa kusajili kifaa chako cha Amazon Fire TV kwa kutumia akaunti yako ya Amazon na nywila.

Taarifa: Utahitaji intaneti kutoka katika kompyuta au kifaa kingine cha mkononi ili kukamilisha hatua hizi.

Kwa habari zaidi kuhusu kifaa hiki, tazama video za Amazon Fire TV zinazoonyesha jinsi ya kuunganisha kifaa hicho.

 Sakinisha programu ya JW Broadcasting kwenye Amazon Fire TV

Nenda kwenye ukurasa wa mwanzo wa Amazon Fire TV, ili usakinishe JW Broadcasting ukitumia hatua zifuatazo:

  • Bofya kwenda Juu au Chini kwa kutumia kibonyezo cha Amazon Fire TV mpaka upate sehemu iliyoandikwa Tafuta.

  • Bonyeza Chagua.

Sehemu ya Tafuta ya Fire TV inatumika kupata sinema, vipindi vya TV, waigizaji, waongozaji wa sinema, programu, michezo na vipindi vingine kulingana na neno unaloandika. Ili kupata programu ya JW Broadcasting nenda kwenye matokeo ya kutafuta ya Ingiza Programu na Michezo. Andika maneno jw broadcasting katika sehemu hiyo.

Maneno JW Broadcasting yanapotokea kwenye orodha ya matokeo, bonyeza kishale kwenda Chini ili uliwekee alama neno hilo JW Broadcasting, kisha bonyeza Chagua. Peleka kishale upande wa Kulia mpaka upate programu, halafu bonyeza Chagua. Bonyeza kitufe kilichoandikwa Pakua(Get) ili upakue programu kwenye kifaa chako cha Amazon Fire TV. Baada ya kupakua programu hiyo sehemu ya kibonyezo hicho cha Pakua kitaweza kutumika kama kitufe cha Fungua.

Ili kutazama JW Broadcasting, chagua Fungua, au nenda kwenye ukurasa wa mwanzo wa Amazon Fire TV na utafute JW Broadcasting kwenye sehemu ya Programu. Tazama sehemu iliyoandikwa Maktaba Yangu ya Programu.