Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

JW BROADCASTING

Sikiliza Audio Kupitia Roku

Sikiliza Audio Kupitia Roku

Sehemu ya Audio ina muziki, drama, na drama za usomaji wa Biblia.

(Taarifa: Kifaa chako cha kubadili vipindi cha Roku kinaweza kuwa tofauti na kinachoonyeshwa kwenye michoro ya mwongozo huu.)

Chagua Audio ili uone rekodi zilizopo. Fuata maagizo haya ili upate na kusikiliza programu:

 Sikiliza Programu

Kila safu ina programu kadhaa. Jina la kila mkusanyo linaonekana sehemu ya juu.

 • Mishale ya Juu na Chini: Tumia hii kuchagua mkusanyo mpya.

 • Mishale ya Kushoto na Kulia: Tumia hii kuchagua audio zilizopo katika mkusanyo mmoja.

Bofya OK ili uchague programu na uone Maelezo ya Audio.

Chagua mojawapo ya mambo yafuatayo:

 • Endelea: Sehemu hii inatumika ikiwa ulisimamisha audio kabla ya kusikiliza yote. Unapobonyeza sehemu hii utaendelea kusikiliza mahali ulipoachia wakati uliopita.

 • Cheza au Cheza Kuanzia Mwanzo: Cheza audio kuanzia mwanzo.

 • Cheza Zote Katika Kitengo Hiki: Cheza zote katika kitengo alichochagua, kuanzia ile inayoonyeshwa wakati huo. Itaacha kucheza programu zote kwenye kitengo hicho zinapoisha.

Sehemu iliyo chini ya Maelezo ya Audio inaonyesha video nyingine katika kitengo hicho. Bofya Chini ili kwenda kwenye kitengo hicho na Juu ili urudi kwenye Maelezo ya Audio.

 Sikiliza Mkusanyo wa Audio

Zaidi ya kucheza programu mojamoja, unaweza kusikiliza kitengo kizima. Nenda kwenye kitengo unachotaka kusikiliza, kisha uchague mojawapo ya mambo yafuatayo:

 • Cheza Zote: Cheza programu zote katika kitengo hicho, kuanzia ya kwanza.

 • Changanya: Cheza programu zote katika kitengo hicho bila mpangilio wowote.

Itaacha kucheza programu zote kwenye kitengo hicho zinapoisha.

 Cheza, Tua, Peleka Mbele, na Rudisha Nyuma Audio

Unaposikiliza programu, unaweza kutumia njia zifuatazo:

 • Cheza/Simamisha au OK: Simamisha audio. Bofya tena ili kuendelea kusikiliza.

 • Peleka Mbele: Peleka mbele kwa sekunde kadhaa. Shikilia kitufe ili usonge haraka katika programu ya audio. Achilia kitufe ili uendelee kusikiliza.

 • Rudisha Nyuma: Rudisha nyuma kwa sekunde kadhaa. Shikilia kitufe ili urudi mwanzo katika programu ya audio. Achilia kitufe ili uendelee kusikiliza.

 • Nyuma: Bofya ili urudi kwenye sehemu ya Audio.