JW BROADCASTING
Maswali Yanayoulizwa Mara Nyingi—JW Broadcasting (Apple TV)
Huenda umeandika neno ambalo si sahihi. (Ona mwongozo wenye kichwa Sakinisha Programu ya JW Broadcasting kwenye Apple TV.) Au, inawezekana kifaa chako hakina uwezo wa kufungua programu hiyo. JW Broadcasting inapatikana kwenye Apple TV (Toleo la 4).
Unaweza kutumia programu ya JW Broadcasting kwenye Apple TV (Toleo la 4 au ya karibuni zaidi ).
Ikiwa una kompyuta au kifaa cha mkononi cha Apple na Apple TV toleo la zamani, unaweza kutumia AirPlay kutazama video kwenye televisheni yako.
Ili kupata orodha ya lugha zinazopatikana kwenye Apple TV. Fungua sehemu ya Mpangilio katika ukurasa wa mwanzo na utumie sehemu ya Chagua Lugha.
Programu ya JW Broadcasting inapakuliwa na kutumiwa bila malipo.
Unapotumia kwa mara ya kwanza akaunti yako ya Apple kuingia kwenye sehemu ya kutunza programu yaani (iTunes Store, App Store, or iBooks Store), utaombwa ueleze njia utakayotumia ya kutuma malipo, kwa kuwa kuna programu katika sehemu hiyo utakazohitaji kulipia.
Ikiwa huhitaji kuambatanisha njia ya malipo na akaunti yako ya Apple, fuata hatua zilizo kwenye sehemu ya msaada ya Apple.
Unaweza kupata msaada kutoka kwa rafiki anayefahamu vizuri kutumia Apple TV au JW Broadcasting. Ikiwa swali lako linahusiana na Apple TV au akaunti yako, tembelea tovuti ya Apple upate msaada. Ikiwa unahitaji msaada kuhusu programu ya JW Broadcasting, tafadhali wasiliana na ofisi ya tawi iliyo karibu nawe.