Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

JW Broadcasting

JW Broadcasting ni kituo cha televisheni kilicho na habari zenye kujenga kiroho kwa ajili ya familia. Tazama habari zilizotayarishwa kwenye studio ya JW Broadcasting, na pia video kadhaa kutoka kwenye tovuti ya jw.org. Fungua sehemu ya Cheza Video Mfululizo ili ujionee video hizo kwa saa 24 au unaweza kutazama video moja moja kwa kubonyeza sehemu ya Chagua Video. Fungua sehemu ya Rekodi za Kusikiliza (Audio) ili usikilize programu mbalimbali za sauti kama vile muziki, drama, na drama za usomaji wa Biblia.

Tazama mtandaoni kwa kutumia kompyuta, tablet, au simu ya mkononi tovuti ya tv.jw.org. Tazama kupitia televisheni yako kwa kutumia Amazon Fire TV, Apple TV, au king’amuzi cha Roku.

Mfuatano wa Vipindi

 • Video zilizopo katika kila kipindi zinaonyeshwa kwa mfululizo, kwa masaa 24 kila siku kufuatana na ratiba.

 • Tazama vipindi mbalimbali, kutia ndani programu ya Video zilizoteuliwa, Sinema, Watoto, Matineja, Programu na Matukio.

 • Tumia ratiba ya vipindi kujua ni nini kifuatacho.

Video za Karibuni

 • Kila kikundi kina video moja au zaidi.

 • Tazama video moja, au ubonyeze Cheza Zote ili utazame video zote.

 • Unaweza kutua, kucheza, kurudisha nyuma, kupeleka mbele, na kuruka baadhi ya sehemu za video wakati unapozitazama.

Muziki na Rekodi

 • Kuna rekodi nyingiza sauti (miziki, drama za usomaji wa Biblia, na nyingine nyingi).

 • Sikiliza rekodi moja, au bonyeza Cheza Zote ili usikilize zote.

 • Bonyeza Changanya ili usikilize mchanganyiko wa rekodi mbalimbali.

 

Njia za Kutazama JW Broadcasting

 • Programu ya TV.JW.ORG: inaweza kufunguka kwenye kompyuta, tablets, na simu za kisasa ziliunganishwa na intaneti na zenye JavaScript. Ikiwa kompyuta yako au kifaa kingine kinacheza video zilizopo katika Tovuti ya jw.org, utaweza pia kutumia programu ya tv.jw.org.

 • Roku app: Roku LT, Roku 1, Roku 2, Roku 3, Roku Streaming Stick.

 • Google Chromecast: Unaweza kutuma video kutoka katika kivinjari cha Chrome kwenda kwenye TV iliyounganishwa na kifaa cha Chromecast.

 • Apple TV app: Apple TV (kizazi cha 4).

 • Amazon Fire TV app:  Amazon Fire TV na Fire TV Stick.