Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

JW BROADCASTING

Maswali Yanayoulizwa Mara Nyingi​—JW Broadcasting (Fire TV)

Maswali Yanayoulizwa Mara Nyingi​—JW Broadcasting (Fire TV)

Huenda umekosea kuandika jina la programu unayotafuta. (Tazama mwongozo Sakinisha Programu ya JW Broadcasting Kwenye Amazon Fire TV.) Au, huenda kifaa chako hakiwezi kucheza programu hiyo. JW Broadcasting inaweza kucheza kwenye Amazon Fire TV na Amazon Fire TV Stick.

 

Unaweza kupata programu ya JW Broadcasting kwenye Amazon Fire TV na Amazon Fire TV Stick.

 

Ili kupata orodha ya lugha zinazopatikana kwenye Amazon Fire TV. Fungua sehemu ya Mpangilio katika ukurasa wa kwanza wa skrini yako na kisha teua sehemu ya Chagua Lugha.

 

Programu ya JW Broadcasting inapakuliwa na kutumiwa bila malipo.

 

Unahitaji kuonyesha njia utakayotumia kutoa malipo ya akaunti yako ya Amazon ili uweze kununua programu. Ili upate programu za bure, tembelea Sehemu ya Msaada na Huduma kwa Wateja ya Amazon.

 

Unaweza kupata msaada kutoka kwa rafiki anayefahamu vizuri kutumia Amazon Fire TV au JW Broadcasting. Ikiwa swali lako linahusiana na kifaa au akaunti ya Amazon Fire TV , Tembelea tovuti ya Amazon ili upate msaada. Ikiwa unahitaji msaada kuhusu programu ya JW Broadcasting, tafadhali wasiliana na ofisi ya tawi iliyo karibu nawe.