Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

JW BROADCASTING

Sakinisha Programu ya JW Broadcasting Kwenye Apple TV

Sakinisha Programu ya JW Broadcasting Kwenye Apple TV

Ili kutazama JW Broadcasting kupitia Apple TV, unahitaji kuunganisha kifaa chako na kusakinisha programu ya JW Broadcasting. Fuata hatua zifuatazo:

 Unganisha Apple TV

Kifaa chako cha Apple TV kinapaswa kuwa na mwongozo utakaokusaidia kukitumia na kuunganisha kwenye intaneti. Apple TV itakapokuwa imeunganishwa, malizia kwa kufuata maagizo yatakayoonyeshwa kwenye skrini.

 Sakinisha Programu ya JW Broadcasting Kutoka Kwenye Sehemu ya Kupakua Programu

Itafute programu ya JW Broadcasting, kisha isakinishe kwa kutumia hatua zifuatazo:

  • Telezesha kidole Upande wa Kulia wa skrini ya kibonyezo chako cha kutafuta vipindi (Siri Remote) mpaka upate neno Tafuta.

  • Bofya kwenye neno hilo Tafuta, kisha tumia herufi zilizojitokeza kuandika neno “JW Broadcasting.”

  • Njia nyingine ni kubonyeza kitufe cha “Siri” na kusema maneno “JW Broadcasting.”

  • Weka alama programu na uibofye kwenye skrini ya kibonyezo.

Sakinisha programu kwa kufuata maelezo yatakayotolewa kwenye skrini.