Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Hamia kwenye yaliyomo

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

JW BROADCASTING

Chagua Video Kupitia Apple TV

Chagua Video Kupitia Apple TV

Sehemu ya Chagua Video inakuruhusu utazame kila video katika JW Broadcasting ukiwa na uwezo wa kusimamisha kwa muda, kupeleka mbele, na kutafuta nyingine. Tazama video moja au video zote kwenye mkusanyo.

(Taarifa: Mwonekano wa kibonyezo cha kubadili vipindi unaoonyeshwa kwenye miongozo hii unaweza usifanane na kibonyezo chako.)

Tafuta kwenye Chagua Video iliyopo kwenye ukurasa wa mwanzo ili kuona vipengele mbalimbali vya video vinavyopatikana. Fuata hatua zifuatazo kutafuta na kutazama video:

 Tafuta Video

 • Tumia kibonyezo chako (Siri Remote) kuchagua vipengele. Kipengele utakachochagua kitakuwa na picha kubwa kuliko vingine.

 • Bonyeza kipengele ulichochagua.

Baadhi ya video zinapatikana katika vipengele mbalimbali. Kwa mfano, video ya Mwana Mpotevu Arudi, inapatikana kwenye kipengele cha Sinema, Familia na Vijana.

Kila kipengele kina mkusanyiko wa video. Jina la kipengele litaonekana juu ya kipengele hicho.

Taarifa: Baadhi ya mikusanyo ya video huendelea upande wa kulia wa skrini.

 • Telezesha Juu au Chini ili kupata mkusanyo mwingine.

 • Telezesha Kushoto au Kulia ili kupata video utakayo kwenye mkusanyo.

 • Kila mkusanyiko wa video una sehemu ya Cheza Zote. Unaweza kuchagua cheza zote ili utazame video zote katika mkusanyiko ukianzia video ya kwanza. Video zinapomaliza kuchezwa kwenye mkusanyo huu zitasimama kucheza.

 • Chagua video ili kuona sehemu ya Maelezo ya Video.

Chagua mojawapo ya mambo haya:

 • Cheza: Cheza video kutoka mwanzo.

 • Cheza Zote: Cheza video zote kwenye mkusanyo huu, kuanzia video inayoonekana kwenye skrini. Video zinapomaliza kuchezwa kwenye mkusanyo huu zitaacha kucheza.

 • Anza Tena: Anza tena video kutoka mahali ulipoishia kutazama.

Kipengele chini ya sehemu ya Maelezo ya Video inaonyesha mikusanyo mingine ya video inayoonekana kwenye skrini. Bonyeza Chini ili kuingia kwenye kipengele hicho, na Juu ili kurudi kwenye sehemu ya Maelezo ya Video.

 Tua, Peleka mbele, Rudisha nyuma video

Unapotazama video kwenye sehemu ya Chagua Video, unaweza kutumia kibonyezo cha kubadili kipindi cha Siri (Siri Remote) kama ifuatavyo:

 • Cheza/Tua: Simamisha kwa muda video. Bonyeza kitufe hicho hicho kuanza tena. Pia unaweza kubonyeza sehemu ya kati ya kibonyezo ili kucheza au kusimamisha kwa muda.

 • Rudisha Nyuma: Telezesha upande wa Kushoto wakati umesimamisha kwa muda video ili kurudi mpaka mwanzo wa video. Bonyeza kitufe cha Cheza/Tua ili kuendelea kucheza.

 • Peleka Mbele: Telezesha upande wa Kulia wakati umesimamisha kwa muda video ili kupeleka mbele video. Bonyeza kitufe cha Cheza/Tua ili kuendelea kucheza.

 • Hatua Mbele: Ili kurusha video mbele kwa sekunde kumi, weka kidole chako kwenye upande wa kulia wa sehemu ya kutelezesha ya kibonyezo chako.

 • Unapoona alama ya Kurusha imetokea kwenye sehemu ya chini ya skrini, bonyeza sehemu ya Kutelezesha.

 • Hatua Nyuma: Ili kurusha video nyuma kwa sekunde kumi, weka kidole chako kwenye upande wa kushoto wa sehemu ya kutelezesha ya kibonyezo chako.

 • Unapoona alama ya Kurusha imetokea kwenye sehemu ya chini ya skrini, bonyeza sehemu ya Kutelezesha.

 • Menyu: Rudi kwenye sehemu ya Maelezo ya Video.

 Tazama Video za Karibuni au Zilizoteuliwa

Ukurasa wa mwanzo wa JW Broadcasting una orodha mbili za pekee za mkusanyo wa Chagua Video:

 1. Zilizoteuliwa: Video hizi ni kwa ajili ya mambo fulani hususa, kama vile zile zilizoteuliwa kwa ajili ya mikutano yetu ya kila juma au ibada ya familia.

 2. Video za Karibuni: Video zilizoongezwa hivi karibuni.