Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

JW BROADCASTING

Tazama Video za Karibuni Kupitia Roku

Tazama Video za Karibuni Kupitia Roku

Unaweza kucheza, kutua, kupeleka mbele, kurudisha nyuma, na kuruka unapotaza video. Tazama video moja au video zote zilizopo.

(Taarifa: Kifaa chako cha kubadili vipindi cha Roku kinaweza kuwa tofauti na kinachoonyeshwa kwenye mwongozo huu.)

 Tafuta na Ucheze Video

Chagua sehemu ya Video iliyo mwanzoni mwa kurasa ili kuona video zilizopo katika sehemu hiyo. Pitia vipengele vya menyu kwa kutumia mishale iliyo kwenye kifaa chako cha kubadili vipindi. Bonyeza kitufe cha OK kuchagua kipengele hicho.

Baadhi ya video zinapatikana chini ya vipengele mbalimbali. Kwa mfano, video ya Mwana Mpotevu Arudi inapatikana katika Sinema, Familia, na Matineja.

Chagua neno Changanya ili kucheza video zote katika kipengele kimoja kwa mfululizo bila kuzingatia mpangilio ulio kwenye orodha.

Kila kipengele kina orodha yenye video nyingi. Kila orodha inawakilisha mkusanyo wa video. Jina la mkusanyo linaonekana juu ya orodha.

Tumia kifaa chako cha kubadili vipindi kuchagua video katika mkusanyo:

 • Mishale ya Juu na Chini: Tumia hii kuhama kwenda kwenye mkusanyo mwingine wa video.

 • Mishale ya Kushoto na Kulia: Tumia hii kuchagua video zilizopo katika mkusanyo mmoja.

Kuna njia mbili za kutazama video katika mkusanyo:

 • Kila mkusanyo una sehemu ya Cheza Zote. Chagua sehemu hiyo ili kucheza video zote katika mkusanyo, kuanzia video ya kwanza. Vipindi vitaacha kuonyeshwa punde tu unapomaliza video ya mwisho katika mkusanyo.

 • Chagua neno Changanya ili kucheza video zote katika kipengele kimoja kwa mfululizo unaofuatana au usiofuatana.

Taarifa: Video zilizopo zikiisha itaacha kucheza.

Chagua video ili kuona Maelezo ya Video.

 • Endelea: Sehemu hii inatumika ikiwa ulisimamisha video kabla ya kufikia mwisho wake. Unapobonyeza sehemu hii unaendelea kutazama video kuanzia sehemu ulipoishia kutazama video hiyo.

 • Cheza au Cheza Kuanzia Mwanzo: Cheza video kuanzia mwanzo.

 • Cheza Pamoja na Maandishi: Sehemu hii inapatikana tu ikiwa maandishi yanapatikana katika video hiyo. Unapoichagua, unatazama video ikiwa na maandishi na yanaweza kuonekana (ikiwa maandishi yapo). Ili kutoa maandishi, bonyeza Cheza Bila Maandishi.

 • Cheza Zote Katika Kitengo Hiki: Cheza video zote katika mkusanyo, ukianza na uliyochagua. Vipindi vitaacha kuonyeshwa punde tu unapomaliza video ya mwisho katika mkusanyo.

Safu iliyo chini ya Maelezo ya Video inaonyesha video nyingine katika mkusanyo huo. Bonyeza kuelekea Chini ili kuingia kwenye safu ya mkusanyo, bonyeza kuelekea Juu ili kurudi kwenye sehemu ya Maelezo ya Video.

 Cheza, Tua, Peleka Mbele, na Rudisha Nyuma Video

Video inapocheza kwenye sehemu ya Chagua Video, unaweza kudhibiti video hiyo kwa kutumia kifaa chako cha kubadili vipindi kama ifuatavyo:

 • Cheza/Simamisha: Sitisha video. Bonyeza kitufe hicho ili video iendelee kucheza.

 • Kulia: Peleka mbele kwa sekunde chache. Endelea kushika kitufe kupeleka mbele video kwa haraka. Video inapofika sehemu unayohitaji kutazama, bonyeza kitufe cha Cheza au kitufe cha OK.

 • Peleka Mbele: Peleka mbele video. Video inapofika sehemu unayohitaji kutazama, bonyeza kitufe cha Cheza au kitufe cha OK.

 • Kushoto: Rudisha nyuma video kwa sekunde chache. Endelea kushika kitufe ili kurudisha nyuma video haraka kuelekea mwanzo wa video. Video inapofika sehemu unayohitaji kutazama, bonyeza kitufe cha Cheza au kitufe cha OK.

 • Rudisha Nyuma: Rudisha nyuma kuelekea mwanzo wa video. Video inapofika sehemu unayohitaji kutazama, bonyeza kitufe cha Cheza au kitufe cha OK.

 • Nyuma: Rudi kwenye sehemu ya Maelezo ya Video..

 Tazama Video Zinazotangulizwa au za Karibuni

Ukurasa wa mwanzo wa JW Broadcasting una mikusanyo miwili ya Video za Karibuni:

 1. Zilizoteuliwa: Ina Video zilizoteuliwa, kama zile zitakazotumiwa katika mikutano yetu ya kila juma au ibada ya familia..

 2. Video za Karibuni: Video zilizoongezwa hivi karibuni.