Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

JW BROADCASTING

Chagua Video Kupitia Amazon Fire TV

Chagua Video Kupitia Amazon Fire TV

Unaweza kutazama video yoyote na kuwa na uwezo wa kuicheza, kutua, kuipeleka mbele, kuirudisha nyuma, na kuiruka. Tazama video moja au video zote zilizopo.

(Taarifa: Mwonekano wa kifaa cha kubadili vipindi unaoonyeshwa kwenye miongozo hii unaweza usifanane na kifaa chako.)

 Tafuta na Tazama Video

Chagua sehemu ya Video iliyo mwanzoni mwa kurasa ili kuona video zilizopo katika sehemu hiyo. Pitia vipengele vya menyu kwa kutumia mishale iliyo kwenye kifaa chako cha kubadili vipindi. Bonyeza kitufe cha Chagua kuchagua kipengele hicho.

Baadhi ya video zinapatikana katika vipengele mbalimbali. Kwa mfano, video ya Mwana Mpotevu Arudi inapatikana kwenye kipengele cha Sinema, Familia na Vijana.

Chagua Changanya ili kucheza video zote katika kipengele kimoja kwa mfululizo bila kuzingatia mpangilio ulio kwenye orodha.

Kila kipengele kina mkusanyo wa video. Jina la kipengele litaonekana juu ya kipengele hicho.

Tumia kifaa cha kubadili vipindi kutafuta mkusanyiko:

 • Juu na Chini: Tafuta mkusanyo mwingine.

 • Kushoto na Kulia: Tafuta video kwenye mkusanyo wa video.

Kuna njia mbili za kutazama video katika mkusanyo:

 • Kila mkusanyo wa video una sehemu ya Cheza Zote. Unaweza kuchagua cheza zote ili utazame video zote katika mkusanyo ukianzia video ya kwanza.

 • Chagua Changanya ili kucheza video zote katika mkusanyo mmoja kwa mfululizo bila kuzingatia mpangilio ulio kwenye orodha.

Taarifa: Video zinapomaliza kuchezwa kwenye mkusanyo huu zitaacha kucheza.

Chagua video ili kuonyesha Maelezo ya Video kwenye skrini.

Chagua mojawapo ya mambo haya kwenye skrini:

 • Cheza: Cheza video kutoka mwanzo.

 • Cheza Zote: Cheza video zote kwenye mkusanyo huu, kuanzia video inayoonekana. Video zinapomaliza kuchezwa kwenye mkusanyo huu zitaacha kucheza.

 • Anza Tena: Anza tena video kutoka mahali ulipoishia kutazama.

 Kipengele chini ya sehemu ya Maelezo ya Video inaonyesha video nyingine katika mkusanyo unaoonekana. Bonyeza Chini ili kuingia kwenye kipengele hicho, na Juu ili kurudi kwenye sehemu ya Maelezo ya Video.

Tua, Peleka Mbele, Rudisha Nyuma Video

Unapotazama video kwenye sehemu ya Chagua Video, unaweza kutumia kifaa cha kubadili kipindi cha Amazon Fire TV kufanya mambo yafuatayo:

 • Cheza/Tua: Simamisha kwa muda video. Bonyeza kitufe kwa mara nyingine ili kuanza kucheza upya video.

 • Peleka Mbele: Peleka mbele video kwa haraka. Video inapoendelea kwenda mbele kufika mahali unapohitaji kutazama, bonyeza kitufe cha Cheza.

 • Rudisha Nyuma: Rudisha nyuma kuelekea mwanzo wa video. Video inapoendelea kurudi nyuma na kufika mahali unapohitaji kutazama, bonyeza kitufe cha Cheza.

 •   Nyuma: Rudi kwenye sehemu ya Maelezo ya Video.

Tazama Video za Karibuni au Zilizoteuliwa

Sehemu ya ukurasa wa mwanzo wa JW Broadcasting ina orodha mbili za pekee za mkusanyo wa Chagua Video:

 1. Video Zilizoteuliwa: Video hizi ni kwa ajili ya mambo fulani hususa, kama vile zile zilizoteuliwa kwa ajili ya mikutano yetu ya kila juma au ibada ya familia.

 2. Video za Karibuni: Video zilizoongezwa hivi karibuni.