Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Mfano wa Kuigwa—Daudi

Mfano wa Kuigwa—Daudi

Mfano wa Kuigwa—Daudi

Daudi anapenda muziki. Ni mwimbaji hodari na mtungaji stadi. Hata hujitengenezea vyombo vya muziki. (2 Mambo ya Nyakati 7:6) Daudi ana ustadi mwingi sana hivi kwamba mfalme wa Israeli anamwalika akapige muziki katika makao ya mfalme. (1 Samweli 16:15-23) Daudi anakubali. Hata hivyo, haingiwi na kiburi, wala hakubali maisha yake yatawaliwe na muziki. Badala yake, anatumia vipawa vyake kumsifu Yehova.

Je, unapenda muziki? Huenda usiwe mwanamuziki mwenye kipawa, lakini bado unaweza kuiga mfano wa Daudi. Jinsi gani? Kwa kutokubali muziki utawale maisha yako au kukufanya ufikiri na kutenda kwa njia inayomvunjia Mungu heshima. Badala yake, tumia muziki kufanya maisha yako yawe yenye kufurahisha zaidi. Uwezo wa kutunga na kufurahia muziki ni zawadi kutoka kwa Mungu. (Yakobo 1:17) Daudi alitumia zawadi hiyo kwa njia zinazompendeza Yehova. Je, utafanya hivyo pia?