Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Neno Lako Linadumu Milele

Neno Lako Linadumu Milele

Pakua:

  1. 1. Walikuwa watu,

    Wenye hofu ya Mungu.

    Waliouthamini upendo wake mkubwa.

    Ukawakubali, wabebe jina lako.

    Watangazie watu,

    Waujue Ufalme wako.

    Ukawatumia,

    Kulitunza Neno lako.

    Uliona, upendo wao.

    Ukawaambia “Andika.”

    (KORASI)

    Neno lako la kweli,

    Linadumu milele.

    Linanufaisha, linaburudisha.

    N’talishika siku zote.

  2. 2. Oh maadui walishindwa

    Kuwanyamazisha.

    Watu wako wa’minifu,

    Walipenda Neno lako.

    Walikuwa tayari kufa,

    Kuitetea Biblia,

    Kwa imani yao na bidii yao,

    Leo tuna Neno lote.

    (KORASI)

    Basi Neno lako la kweli,

    Linadumu milele.

    Linanufaisha, linaburudisha,

    N’talishika siku zote.

  3. 3. Umetujulisha jina lako,

    Katika Neno lako.

    Wewe ni Yehova,

    Mungu wa milele.

    Tutakusifu milele.

    (KORASI)

    Ni Neno lako la kweli,

    Linadumu milele.

    Linanufaisha, linaburudisha.

    N’talishika sikuzote,

    Sikuzote.