Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Mazungumzo ya Familia

Mazungumzo ya Familia

Mazungumzo ya Familia

Kuna Kasoro Gani Katika Picha Hii?

Soma Mwanzo 24:1-4, 10-23. Ni mambo gani matatu katika picha hii ambayo si sahihi? Andika majibu yako kwenye mistari iliyo hapa chini, na ukamilishe picha hii kwa kuipaka rangi.

1. ․․․․․

2. ․․․․․

3. ․․․․․

ZUNGUMZENI PAMOJA:

Ni sifa zipi muhimu ambazo Rebeka alionyesha?

DOKEZO: Soma Methali 31:17, 27, 29-31; 1 Petro 4:9.

Unaweza kumwigaje Rebeka?

DOKEZO: Soma Methali 11:25; Waroma 12:11.

UTENDAJI WA FAMILIA:

Andika jina la mtu ambaye ungependa kumsaidia. Halafu, andika orodha ya mambo ambayo ungependa kumfanyia. Waonyeshe watu wa familia karatasi yako. Amueni pamoja mambo mtakayomfanyia mtu huyo na ni lini mtafanya hivyo. Baada ya kumsaidia, ketini na mzungumzie jinsi mlivyohisi kwa kufanya jambo hilo.

Kusanya na Ujifunze

Kata, kunja katikati, na uhifadhi

KADI YA BIBLIA 13 AYUBU

MASWALI

A. Kwa ujumla, Ayubu alikuwa na wana ․․․․․ na binti ․․․․․.

B. Shetani alichukua nini kutoka kwa Ayubu?

C. Kamilisha maneno ya Ayubu: “Mpaka nitakapokata pumzi, sitajiondolea . . .”

[Chart]

4026 K.W.K. 1 W.K. 98 W.K.

Adamu aumbwa Aliishi karibu na Kitabu cha mwisho cha

1600 K.W.K Biblia kinaandikwa

[Ramani]

Aliishi nchi ya Uzi

NCHI YA AHADI

MISRI

UZI?

AYUBU

MAMBO MACHACHE KUMHUSU

Mwanamume “asiye na lawama na mnyoofu” machoni pa Mungu. (Ayubu 1:8) Ingawa mke wake na watu wengine walimshinikiza, Ayubu hakuacha kumtumikia Mungu. (Ayubu 1:20-22; 2:9, 10) Uvumilivu wake na matokeo mazuri aliyopata hutupatia ujasiri wa kuvumilia majaribu kwa ushikamanifu.​—Ayubu 42:12-17; Yakobo 5:11.

MAJIBU

A. 14, 6.—Ayubu 1:2; 42:13.

B. Mifugo, watumishi, watoto, na afya yake.​—Ayubu 1:13-19; 2:4-7.

C. “. . . utimilifu wangu!”​—Ayubu 27:5.

Watu na Nchi

4. Jina langu ni Lukas. Nina umri wa miaka saba, na ninaishi nchini Ujerumani. Kuna Mashahidi wangapi wa Yehova nchini Ujerumani? Ni 60,000, 100,000, au 160,000?

5. Ni alama gani inayoonyesha eneo ninaloishi? Chora duara kuzunguka alama hiyo, na uchore alama nyingine kuonyesha eneo unaloishi kisha uone kwenu ni umbali gani kutoka Ujerumani.

A

B

C

D

Watoto Watafute Picha

Je, unaweza kupata picha hizi katika toleo hili? Kwa maneno yako mwenyewe, eleza jambo linalotendeka katika kila picha.

Ili uchapishe nakala zaidi za “Mazungumzo ya Familia,” nenda kwenye www.jw.org

● Majibu ya “MAZUNGUMZO YA FAMILIA” kwenye ukurasa wa 27

MAJIBU YA UKURASA WA 30 NA 31

1. Kunapaswa kuwa na ngamia 10, na si 11.

2. Rebeka alijaza maji ndani ya chombo cha kunyweshea wanyama si katika mapipa matatu.

3. Mtumishi alimpa Rebeka pete ya puani na vikuku viwili kwa ajili ya mikono yake, wala si ushanga.

4. 160,000.

5. C.