Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Magonjwa Yanayoenezwa na Wadudu Mimi ni mwalimu katika chuo kikuu na nimekuwa nikisimamia maabara ya elimu ya viini, vimelea, na biokemia kwa miaka 24 iliyopita. Nyinyi huzungumzia mambo ya kisayansi kwa njia rahisi! Mfululizo “Magonjwa Yanayoenezwa na Wadudu” ulinipendeza. (Mei 22, 2003) Nyakati nyingine sielewi mambo fulani katika vitabu vya kisayansi. Lakini mnapoyazungumzia, mimi huyaelewa haraka. Asanteni kwa jitihada zenu zote.

M. R., Mexico

Kuiba Mtihani Asanteni kwa makala “Vijana Huuliza . . . Kuna Ubaya Gani Kuiba Mtihani?” (Januari 22, 2003) Wanafunzi wenzangu wametaka kunilipa pesa nyingi sana ili niwafanyie mtihani. Kwa kukataa kuiba mtihani nimedhaniwa kuwa mpumbavu. Makala hiyo ilinikumbusha kutetea kanuni za Mungu bila kuyumbayumba.

F.A.C., Nigeria

Sikuwa nikifanya kazi za shule kamwe, bali nilikuwa nikiiba kazi ya wanafunzi wenzangu darasani. Makala hiyo ilinisaidia kuelewa kwamba kuiba kazi ya mwingine ni wizi. Ijapokuwa wanafunzi wenzangu hawakubali maoni hayo, nimeamua kuchukua msimamo.

Y. D., Urusi

Basi la Umeme Mimi huishi na kufanya kazi Italia, na ninamthamini sana mwanamke mmoja, Shahidi wa Yehova, ambaye huniletea magazeti yenu ya lugha ya Kirusi. Nilisoma makala “Safari Ndefu Zaidi kwa Basi la Umeme.” (Machi 22, 2003) Ilizungumzia pwani ya Krimea, ambako niliishi zamani. Asanteni kwa masimulizi hayo mafupi kuhusu nyumbani kwetu.

Z. B., Italia

Kisukari Niliposoma makala “Kuishi na Kisukari” (Mei 8, 2003) na kuona kwamba kwenda haja ndogo mara nyingi ni dalili ya ugonjwa huo, nilitambua kwamba huenda nina kisukari. Kwa hiyo nilienda hospitalini nikapata kwamba ninaugua kisukari. Mwezi mmoja umepita tangu nilipochunguzwa, na ninajitahidi kupunguza kiasi cha sukari katika damu yangu kwa kutumia dawa, kuboresha lishe, na kufanya mazoezi. Ikiwa singeona gazeti hilo, singejua kwamba nina ugonjwa huo.

Y. N., Japan

Mimi si Shahidi wa Yehova, lakini mimi hupata magazeti yenu kutoka kwa jirani mwenye fadhili. Nilifurahia sana makala kuhusu kisukari. Kwa kuwa ninasomea jinsi ya kuwauguza wazee, ilinibidi niandike insha kuhusu habari hiyo. Ikiwa ningepokea gazeti hilo siku chache mapema, singefanya utafiti katika vitabu vingi sana! Makala zenu zina faida nyingi.

A. S., Ujerumani

Minyoo Nilifurahia makala “Minyoo wa Ajabu.” (Mei 8, 2003) Nilikuwa nikisikiliza redio wakati niliposikia habari fulani kuhusu minyoo. Nilichukua gazeti langu la Amkeni! mara moja na kufungua makala hiyo. Kwa kushangaza, mtangazaji wa redio alikuwa akinukuu gazeti hilo. Hilo lilinionyesha kwamba Amkeni! lina faida ulimwenguni pote.

F. B., Nigeria

Nilishangaa niliposoma kwamba kuna zaidi ya aina 1,800 za minyoo. Ikiwa viumbe hao hawangekuwa wakitengeneza udongo, tungekuwa tukilima udongo mgumu mchana kutwa. Hata hivyo, makala hiyo haikunifanya niwapende minyoo, lakini ninaelewa faida yao.

Y. N., Japan