Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Joto Hupunguza Ambukizo

Joto Hupunguza Ambukizo

Joto Hupunguza Ambukizo

MARA NYINGI WATU WANAOPASULIWA HUPATA AMBUKIZO katika kidonda. Hata hivyo, gazeti la The Times la London linaripoti kwamba “joto linaweza kupunguza uwezekano wa watu waliopasuliwa kupata ambukizo kwa zaidi ya asilimia 60.”

Watafiti kwenye Hospitali ya Chuo Kikuu cha North Tees, Uingereza, waliwagawanya katika vikundi vitatu wagonjwa 400 waliohitaji kufanyiwa upasuaji wa matiti, au kwa sababu ya mishipa iliyovimba au ngiri. Wagonjwa wa kikundi kimoja walikuwa na joto la kawaida, lakini mbinu za kupasha joto kwenye sehemu fulani za mwili au mwili mzima zilitumiwa kwa ajili ya vikundi vile vingine viwili. Hizo zilitumiwa kwa muda wa nusu saa kabla ya upasuaji. Matokeo yakawa nini?

Baada ya upasuaji, asilimia 5 tu ya wale waliofaidika kwa mbinu za kupasha joto walipata ambukizo, hali asilimia 14 ya wale ambao hawakufaidika kwa mbinu hiyo walipata ambukizo. Tayari matokeo yanaonyesha kwamba joto limepunguza ambukizo katika watu wanaofanyiwa upasuaji wa utumbo-mpana.