Kiswahili
JW Library kwa Ajili ya Vifaa vya Windows
https://cms-imgp.jw-cdn.org/img/p/802013033/univ/art/802013033_univ_sqr_xl.jpg

JW Library kwa Ajili ya Vifaa vya Windows

JW Library kwa Ajili ya Vifaa vya Windows

Jifunze kuhusu sehemu mbalimbali za JW Library kwa kutumia madokezo yanayokuonyesha hatua kwa hatua jinsi ya kuitumia. Pata majibu ya maswali yanayoulizwa mara nyingi kuhusu programu hiyo.

 

 

Ni Nini Kipya?

Machi 2026 (Toleo la 15.7)

  • Safu ya habari za utafiti katika Biblia inaonyesha visehemu vya drama Habari Njema Kulingana na Yesu.

  • Baadhi ya matatizo yamerekebishwa kutia ndani yale yaliyosababisha tovuti hiyo kuganda au kutoweka.

Desemba 2025 (Toleo la 15.6)

  • Tumia kitufe cha kutafuta kwenye tabo ya Maktaba ili kupata machapisho, video, na rekodi za sauti kwa kutumia kichwa cha habari unayotafuta.

  • Baadhi ya matatizo yamerekebishwa kutia ndani yale yaliyosababisha tovuti hiyo kuganda au kutoweka.

  • Mifumo ya chini zaidi inayoweza kumudu JW Library sasa ni Android 8.0, iOS 15, macOS iliyo na chipu ya M1 au ya karibuni zaidi, Toleo la 10 la Windows ya 2004 au ya karibuni zaidi.

Oktoba 2025 (Toleo la 15.5)

  • Video na rekodi za sauti zitacheza kwa kasi ileile iliyochaguliwa hata baada ya kuzima na kuwasha programu.

  • Video inapochezwa safu ya taarifa na vidhibiti vinavyoonekana juu ya video hufichwa. Ili safu hiyo ionekane tena utahitaji kubofya video hiyo.

  • Baadhi ya matatizo yamerekebishwa kutia ndani yale yaliyosababisha tovuti hiyo kuganda au kutoweka.

  • Mifumo ya chini zaidi inayoweza kumudu JW Library sasa ni Android 7.0, iOS 15, macOS iliyo na chipu ya M1 au ya karibuni zaidi, Toleo la 10 la Windows ya 2004 au ya karibuni zaidi.

 

KATIKA SEHEMU HII

Anza Kutumia JW Library​—Windows

Jifunze jinsi ya kutumia sehemu mbalimbali muhimu za JW Library kwenye vifaa vyenye mfumo wa Windows.

Pakua na Utumie Biblia​—Windows

Jifunze jinsi ya kupakua na kutumia Biblia katika JW Library kwenye vifaa vya Windows.

Pakua na Utumie Machapisho​—Windows

Jifunze jinsi ya kupakua na kutumia machapisho kwenye JW Library katika vifaa vya Windows.

Tumia Vialamisho, au, Alama za Kukumbuka Ukurasa​—Windows

Jifunze jinsi ya kutumia alama za kukumbuka ukurasa katika vifaa vyenye mfumo wa JW Library.

Tumia Historia​—Windows

Jifunze jinsi ya kutumia sehemu ya historia kwenye JW Library katika vifaa vyenye mfumo wa Windows.

Panga Habari Kulingana na Mapendezi Yako​—Windows

Jifunze jinsi ya kupanga habari kulingana na mapendezi yako kwenye JW Library katika vifaa vyenye mfumo wa Windows.

Tafuta Katika Biblia au Chapisho​—Windows

Jifunze jinsi ya kutafuta katika Biblia au chapisho, na jinsi ya kutafuta habari kuu kutoka kwenye Insight on the Scriptures katika JW Library katika vifaa vyenye mfumo wa Windows.

Tia Alama Maandishi​—Windows

Jifunze jinsi ya kutia alama maandishi kwenye JW Library katika vifaa vyenye mfumo wa Windows.

Sakinisha JW Library Ikiwa Huwezi Kuipakua Kwenye (App Store) Ukitumia Kifaa cha Windows

Ikiwa huwezi kusakinisha JW Library kwenye kifaa chako cha Windows kutoka kwenye app store rasmi, unaweza kuisakinisha kwa kutumia faili za kusakinisha za JW Library Windows.

Maswali Yanayoulizwa Mara Nyingi​—JW Library (Windows)

Pata majibu ya maswali yanayoulizwa mara nyingi.