JW LIBRARY
Kutumia Faili za Media Ulizopakua Awali—Kwenye Windows
Ikiwa ulikuwa umepakua video au rekodi za sauti kwenye toleo la awali la JW Library au JW Library Sign Language katika kifaa kinachotumia Windows, huhitaji kuzipakua tena, unaweza kuendelea kutumia faili ulizokuwa umepakua awali.
JW Library hutafuta faili zozote za media ulizokuwa umepakua kwenye kifaa chako. Inapomaliza kuzitafuta, faili hizo zilizopakuliwa zitapatikana kwenye programu hiyo ya JW Library.
Kwenye Tabo ya Biblia:
Bofya kitufe cha Pakua Media (Download Media)
Chagua Tafuta (Check)
Kwenye Ukurasa wa Yaliyomo Katika Chapisho Lolote:
Bofya kitufe cha Pakua Media (Download Media)

