Kiswahili
JW Library kwa Ajili ya Vifaa vya Android
https://cms-imgp.jw-cdn.org/img/p/802013031/univ/art/802013031_univ_sqr_xl.jpg

JW Library kwa Ajili ya Vifaa vya AndroidTM

JW Library kwa Ajili ya Vifaa vya AndroidTM

Jifunze kuhusu sehemu mbalimbali za JW Library kwa kutumia madokezo yanayokuonyesha hatua kwa hatua jinsi ya kuitumia. Pata majibu ya maswali yanayoulizwa mara nyingi kuhusu programu hiyo.

 

 

Ni Nini Kipya?

Machi 2026 (Toleo la 15.7)

  • Safu ya habari za utafiti katika Biblia inaonyesha visehemu vya drama Habari Njema Kulingana na Yesu.

  • Baadhi ya matatizo yamerekebishwa kutia ndani yale yaliyosababisha tovuti hiyo kuganda au kutoweka.

Desemba 2025 (Toleo la 15.6)

  • Tumia kitufe cha kutafuta kwenye tabo ya Maktaba ili kupata machapisho, video, na rekodi za sauti kwa kutumia kichwa cha habari unayotafuta.

  • Baadhi ya matatizo yamerekebishwa kutia ndani yale yaliyosababisha tovuti hiyo kuganda au kutoweka.

  • Mifumo ya chini zaidi inayoweza kumudu JW Library sasa ni Android 8.0, iOS 15, macOS iliyo na chipu ya M1 au ya karibuni zaidi, Toleo la 10 la Windows ya 2004 au ya karibuni zaidi.

Oktoba 2025 (Toleo la 15.5)

  • Video na rekodi za sauti zitacheza kwa kasi ileile iliyochaguliwa hata baada ya kuzima na kuwasha programu.

  • Video inapochezwa safu ya taarifa na vidhibiti vinavyoonekana juu ya video hufichwa. Ili safu hiyo ionekane tena utahitaji kubofya video hiyo.

  • Baadhi ya matatizo yamerekebishwa kutia ndani yale yaliyosababisha tovuti hiyo kuganda au kutoweka.

  • Mifumo ya chini zaidi inayoweza kumudu JW Library sasa ni Android 8.0, iOS 15, macOS iliyo na chipu ya M1 au ya karibuni zaidi, Toleo la 10 la Windows ya 2004 au ya karibuni zaidi.

 

KATIKA SEHEMU HII

Anza Kutumia JW Library​—Android

Jifunze jinsi ya kutumia sehemu mbalimbali za JW Library kwenye vifaa vya Android.

Pakua na Utumie Biblia​—Android

Jifunze jinsi ya kupakua na kutumia Biblia kwenye JW Library katika vifaa vyenye mfumo wa Android.

Pakua na Utumie Machapisho​—Android

Jifunze jinsi ya kupakua na kutumia machapisho kwenye JW Library katika vifaa vyenye mfumo wa Android.

Tumia Alama za Kukumbuka Ukurasa​—Android

Jifunze jinsi ya kutumia alama za kukumbuka ukurasa kwenye programu ya JW Library katika vifaa vyenye mfumo wa Android.

Tumia Historia​—Android

Jifunze jinsi ya kutumia sehemu ya historia kwenye JW Library katika vifaa vyenye mfumo wa Android.

Panga Habari Kulingana na Mapendezi Yako​—Android

Jifunze jinsi ya kupanga habari kulingana na mapendezi yako kwenye JW Library katika vifaa vyenye mfumo wa Android.

Tafuta Katika Biblia au Chapisho​—Android

Jifunze jinsi ya kutafuta katika Biblia au chapisho, na jinsi ya kutafuta habari kuu kutoka kwenye Insight on the Scriptures katika JW Library katika vifaa vyenye mfumo wa Android.

Tia Alama Maandishi​—Android

Jifunze jinsi ya kutia alama maandishi kwenye JW Library katika vifaa vyenye mfumo wa Android.

Sakinisha JW Library Ikiwa Huwezi Kuipakua Kwenye (App Store) Ukitumia Kifaa cha Android

Ikiwa huwezi kusakinisha JW Library kwenye kifaa chako cha Android kutoka kwenye app store, unaweza kuipakua kwa kutumia JW Library Android Package Kit (APK), na kuisakinisha.

Maswali Yanayoulizwa Mara Nyingi​—JW Library (Android)

Pata majibu ya maswali yanayoulizwa mara nyingi.