Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

WIMBO NA. 93

Bariki Kukutana Kwetu

Bariki Kukutana Kwetu

(Waebrania 10:24, 25)

  1. 1. Ee Yehova tubariki,

    Katika mikutano.

    Twakuomba uwe nasi;

    Utupe roho yako.

  2. 2. Kubali ibada yetu;

    Utufundishe Neno.

    Tuzoeze kuhubiri;

    Na kuwa na upendo.

  3. 3. Ewe Baba twakuomba

    Umoja na amani.

    Kwa maneno na matendo,

    tukweze Enzi yako.