Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

WIMBO NA. 14

Kumsifu Mfalme Mpya wa Dunia

Kumsifu Mfalme Mpya wa Dunia

(Zaburi 2:12)

  1. 1. Kuna umati wa watu,

    toka kila taifa.

    Unakusanywa na Kristo

    na kutaniko lake.

    Ufalme umezaliwa;

    Hivi punde utaanza

    Kutawala dunia yetu,

    Faraja tupate sote.

    (KORASI)

    Msifuni Mungu wetu Yehova;

    Msifuni Kristo Mwana wake.

    Twakubali utawala wake.

    Na kumsifu Kristo.

  2. 2. Kwa nderemo na vifijo,

    Tunamsifu Kristo.

    Twatazamia kwa hamu:

    Dunia Paradiso.

    Awafufuapo wafu,

    Pindi ya kushangilia!

    Hatutaogopa lolote,

    Anapotawala Kristo.

    (KORASI)

    Msifuni Mungu wetu Yehova;

    Msifuni Kristo Mwana wake.

    Twakubali utawala wake.

    Na kumsifu Kristo.