Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

KUUTAZAMA ULIMWENGU

Kuimulika Asia

Kuimulika Asia

Bara la Asia ndilo bara lenye watu wengi zaidi. Zaidi ya theluthi moja ya watu duniani wanaishi China na India. Ni changamoto gani zinazokabili nchi za bara la Asia katika kuelimisha na kulinda raia zao?

Elimu Huwalinda Watoto

Wataalamu wa sheria nchini China wanasema kwamba watoto wanakabili hatari kubwa ya kutendewa vibaya, ikiwa wazazi wao hawatawafundisha kuhusu ngono wakiwa bado wadogo. Katika kipindi cha miaka minne ya hivi karibuni, waendesha mashtaka nchini China walishughulikia mashtaka zaidi ya 8, 000 yaliyohusu watoto waliotendewa vibaya kingono. Profesa wa sheria katika Chuo Kikuu cha Beijing Normal, anasema kwamba watoto “wanaweza kushawishika kwa urahisi. Elimu ndiyo njia kuu ya kuzuia kutendewa vibaya kingono.”

BIBLIA INASEMA NINI? Wazazi wenye hekima huwafundisha watoto wao jinsi ya kujilinda “kutoka kwa mtu anayesema mambo mapotovu.”—Methali 2:1, 10-12.

Vifo Baada ya Kimbunga

Uchunguzi mmoja unaonyesha kwamba kwa wastani, idadi ya wasichana wachanga ambao hufa kwa mwaka baada ya kimbunga kutokea nchini Filipino inazidi ile ya watu wanaokufa kutokana na dhoruba yenyewe, yaani, watu 15 kwa 1. Baadhi ya mambo yanayochangia hali hiyo ni ukosefu wa kazi baada ya dhoruba, gharama za kujenga upya, na pia ugawaji wa misaada kwa watoto wa kike, inayotia ndani chakula na huduma za afya.

BIBLIA INASEMA NINI? ‘Mgawie mwenye njaa mkate wako, na uwaingize nyumbani kwako watu wanaoteseka, wasio na makao. Ukimwona mtu aliye uchi, umfunike.’—Isaya 58:7.

Visa vya Kujiua kwa Wazee Korea Kusini

Katika mwaka wa 2011, zaidi ya robo ya watu waliojiua nchini Korea Kusini walikuwa na umri wa miaka 65 na zaidi. Watafiti fulani wanasema kwamba baadhi ya visababishi vya vifo hivyo ni mitazamo inayobadilika kuhusu kuwatunza wazee na hali za kiuchumi—asilimia 50 hivi ya wazee nchini Korea Kusini ni maskini. Chini ya asilimia hamsini ya watu nchini humo wanasema kwamba watoto wanapaswa kuwategemeza wazazi wao wanaozeeka.

BIBLIA INASEMA NINI? “Mheshimu baba yako na mama yako.” —Waefeso 6:2.