Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

NCHI NA WATU

Kutembelea Honduras

Kutembelea Honduras

NENO Honduras linamaanisha “Kina” katika Kihispania, na huenda Christopher Columbus alitumia neno hilo kuelezea maji yaliyo katika Pwani ya Atlantiki. Baadhi ya watu husema kwamba hivyo ndivyo nchi ya Honduras ilivyopewa jina.

Watu wa Honduras wanathamini sana ushikamanifu na ushirikiano katika familia. Kwa mfano, maamuzi makubwa kama vile gharama za nyumbani au elimu ya watoto, kwa kawaida hufanywa na mume na mke.

Watu wengi wa Honduras ni mchanganyiko wa watu wa Ulaya na wenyeji. Bado kuna makabila ya asili kama vile Wachortí. Makabila mengine yanatia ndani Wagarifuna ambao asili yao si Honduras.

Mwanamuziki Mgarifuna akipiga ngoma iliyotengenezwa kwa mbao ngumu

Wagarifuna walitokana na Waafrika na Wahindi wa kabila la Wakaribu walioishi katika kisiwa cha St. Vincent. Karibu mwaka wa 1797, Wagarifuna waliwasili Islas de la Bahía (Visiwa vya Bay). Baadaye, waliishi katika Pwani ya Karibea katika Amerika ya Kati. Hatimaye, Wagarifuna walitawanyika hadi maeneo mengine ya Amerika ya Kati na Kaskazini.

Wagarifuna wanapenda kucheza dansi ya mdundo wa ngoma zilizotengenezwa kwa mbao ngumu. Utamaduni wao unatia ndani pia mavazi ya kitamaduni yenye rangi zinazong’aa, kusimulia hadithi, na chakula kama vile ereba (keki pana na nyembamba iliyotengenezwa kwa unga wa muhogo).

Kuna makutaniko 400 hivi ya Mashahidi wa Yehova nchini Honduras. Mikutano inafanywa katika lugha ya Kichina (Mandarin), Kigarifuna, Kihispania, Kiingereza, Kimiskito, na Lugha ya Ishara ya Honduras.

Ereba, keki pana na nyembamba iliyotengenezwa kwa unga wa muhogo