Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

WIMBO NA. 128

Kuvumilia Mpaka Mwisho

Kuvumilia Mpaka Mwisho

(Mathayo 24:13)

  1. 1. Kwa kuwa tuna ahadi,

    Piga moyo konde.

    Mambo uliyojifunza,

    Ni kweli na hakika.

    Uwe imara katika

    Imani takatifu.

    Dumisha utimilifu;

    Unapojaribiwa.

  2. 2. Usipoteze upendo

    Wako wa mwanzoni.

    Licha ya kujaribiwa,

    Uvumilie yote.

    Hata nini kikupate,

    Usiogope kamwe.

    Yehova atakulinda,

    Yuko karibu nawe.

  3. 3. Watakaovumilia

    Wataokolewa.

    Majina yako katika

    Kitabu cha uzima.

    Basi na tuazimie

    Kuitimiza kazi.,

    Ndipo tupate kibali,

    Chake Yehova Mungu.