Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Fumbo la Masikio ya Wadudu Wadogo Lafumbuliwa

Fumbo la Masikio ya Wadudu Wadogo Lafumbuliwa

Fumbo la Masikio ya Wadudu Wadogo Lafumbuliwa

“Katika muda wa miaka 10 iliyopita, wanabiolojia waligundua utaratibu fulani ambao huwawezesha wanyama kutambua upande ambao sauti zinatoka,” lasema gazeti la Science News. “Waligundua jambo hilo baada ya kumchunguza mdudu anayewinda nyenje kwa kufuata sauti yao, hata ingawa kichwa cha mdudu huyo ni kidogo mno kuweza kusikia sauti kwa njia za kawaida.” Kwa kawaida utaratibu huo hutegemea umbali uliopo kati ya viwambo vya masikio.

Kulingana na uchunguzi wa hivi karibuni uliofanywa kwenye Chuo Kikuu cha Cornell, Marekani, “wadudu wa kike wa jamii ya Ormia ochracea hutambua upande ambao sauti zinatoka kwenye eneo lenye ukubwa wa nyuzi 2 kama vile tu bundi afanyavyo,” ijapokuwa urefu wa viwambo vyao vya masikio hauzidi milimeta moja! Mdudu huyo anaweza kusikia kwa njia bora kama bundi kwa sababu ya muundo wa kipekee wa sikio lake.

Viwambo vya masikio ya mdudu huyo vimeunganishwa na utando ambao unaviwezesha kubembea-bembea. Sauti ya nyenje inapofika kwenye kiwambo kilicho karibu, mitikiso ya kiwambo hicho huwasilishwa mara moja kwenye kiwambo cha pili. Lakini mitikiso inayofika kwenye kiwambo cha pili huwa hafifu. Kwa hiyo, kiwambo kilicho karibu na nyenje hutikisika kwa nguvu zaidi na kumwezesha mdudu huyo kujua mahali hususa lilipo windo lake.

Ugunduzi huo una manufaa gani? Watafiti wanaamini kwamba unaweza kuwasaidia kuboresha muundo wa vifaa kama vile vikuza-sauti na vifaa vya kuwasaidia watu kusikia vizuri. Ripoti hiyo yasema kwamba vifaa hivyo vinaweza kuundwa ili “kumsaidia mtu kusikia sauti hasa kutoka upande anaotazama.” Kwa kweli, uumbaji wa ajabu wa Yehova unadhihirisha hekima isiyo na kifani!—Ayubu 42:2.

[Hisani]

R. Hoy/Cornell University

Top two photos: R. Wyttenbach/ Cornell University