Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Mahakama ya Juu Yakubali Kusikiliza Kesi

Mahakama ya Juu Yakubali Kusikiliza Kesi

Mahakama ya Juu Yakubali Kusikiliza Kesi

KATIKA MIAKA YA HIVI MAJUZI, Mahakama ya Juu imekubali kusikiliza kesi 80 hadi 90 tu kila mwaka kati ya maombi zaidi ya 7,000 yanayofanywa. Hiyo ni asilimia 1 hivi ya maombi yote. Katika kesi hizo Mahakama hiyo hutoa hati rasmi inayoonyesha sababu za uamuzi wake.

Mnamo Mei 2001, Mashahidi wa Yehova waliwasilisha Maombi ya Hati ya Kuhawilisha Kesi (ruhusa ya kusikiliza tena kesi) kwenye Mahakama ya Juu, wakiuliza hivi: “Je, ni kweli kwamba kulingana na katiba wahudumu wa kidini wanaofanya kazi ya kueleza imani yao nyumba hadi nyumba ambayo inapatana na Maandiko na ambayo imefanywa kwa karne nyingi, wako sawa na wachuuzi wa bidhaa, na wanapaswa kupata kibali kutoka kwa manispaa ili kuongea kuhusu Biblia au kutoa vichapo vyao vya Biblia bila malipo?”

Mnamo Oktoba 15, 2001, Idara ya Sheria ya Watchtower ilifahamishwa kwamba Mahakama ya Juu ya Marekani imekubali kusikiliza upya kesi ya Watchtower Bible and Tract Society of New York, Inc., et al. v. Village of Stratton et al!

Mahakama ilikubali kusikiliza kesi hiyo kwa msingi wa suala linalohusiana hasa na uhuru wa kusema, yaani, ikiwa kweli haki za uhuru wa kusema zilizo katika Marekebisho ya Kwanza ya Katiba ya Marekani zinatia ndani haki ya watu ya kuongea na wengine juu ya jambo fulani bila kuhitaji kujitambulisha kwa wawakilishi wa serikali.

Sasa mjadala wa kesi hiyo ungefanywa mbele ya majaji tisa wa Mahakama ya Juu ya Marekani. Mashahidi walileta mawakili wao, na Kijiji cha Stratton kilikuwa pia na mawakili. Ikawaje?

[Sanduku katika ukurasa wa 5]

MAREKEBISHO YA KWANZA NI NINI?

“MAREKEBISHO YA KWANZA (KUANZISHA DINI; UHURU WA DINI, WA KUSEMA, WA KUSAMBAZA HABARI, WA KUKUSANYIKA, WA KUWASILISHA MAOMBI) Bunge halitatunga sheria yoyote kuhusiana na kuanzisha dini, wala kuwazuia watu kufuata dini kwa uhuru; wala kuwanyima uhuru wa kusema au wa kusambaza habari; au haki ya kukusanyika kwa amani, na kuomba Serikali iondoe kisababishi cha malalamiko yao.”—The U.S. Constitution (Katiba ya Marekani).

“Marekebisho ya Kwanza ndiyo msingi wa demokrasia nchini Marekani. Marekebisho ya Kwanza yanazuia Bunge kutunga sheria zinazodhibiti uhuru wa kusema, wa kusambaza habari, wa kukusanyika kwa amani, au wa kuwasilisha maombi. Watu wengi huonelea kwamba uhuru wa kusema ndiyo uhuru muhimu zaidi na msingi wa uhuru mwingine wowote. Marekebisho ya Kwanza pia yanazuia Bunge kutunga sheria ya kuanzisha dini ambayo inaungwa mkono na serikali au kuzuia uhuru wa dini.” (The World Book Encyclopedia) Yafaa kutambua kwamba uamuzi muhimu ulifanywa pia kuhusiana na Mashahidi wa Yehova katika kesi ya Cantwell v. Connecticut, 310 U.S. 296 (1940), wakati Mahakama ya Juu ya Marekani ilipoamua kwamba haki zilizo katika Marekebisho ya Kwanza zinazuia “Bunge la Marekani” (serikali) na vilevile mamlaka za mitaa (za serikali na za manispaa) kutunga sheria ambazo zitaingilia haki za Marekebisho ya Kwanza isivyo halali.

[Picha katika ukurasa wa 5]

Suala lililohusika linaathiri shughuli mbalimbali za kwenda nyumba hadi nyumba

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 4]

Photograph by Franz Jantzen, Collection of the Supreme Court of the United States